Kupotea kwa Ndege ya MH370: Waziri Mkuu wa Australia Ajichanganya

Ocean Shield deploys the Bluefin 21 underwater vehicle

Kifaa cha kutafutia mabaki ya ndege iliyopotea kikiwa baharini
Ukurasa rasmi wa Flickr wa Jeshi la Majini la Marekani[CC-BY-2.0]

Waziri Mkuu wa Australia Tony Abbott hayuko peke yake katika kuusaka umaarufu wa kimataifa. Mtangulizi wake Kevin Rudd alipenda sana kusikika duniani kote. Hata hivyo, jaribio lake la hivi karibuni la kujaribu kina cha maji cha siasa hatari za kutafutwa kwa ndege iliyopotea liliwasha moto wa wakosoaji wake.

Zoezi la kutafuta ndege hiyo ya shirika la ndege la Malaysia yenye namba MH370 limekuwa likiendelea kwenye bahari ya hindi kuelekea magharibi mwa Perth. Huku akimwulikwa na vyombo vya habari vya dunia wakati wa ziara yake nchini China, Abbott kwa furaha kabisa alitangaza tarehe 12 Aprili 2014 kwamba:

Tuna uhakika kwamba tunajua welekeo wa kifaa cha taarifa za ndege hiyo (black box) kwa umbali wa kilometa kadhaa, lakini uhakika wa mahali kilipo kifaa hicho si sawa na kuokoa mabaki ya ndege hiyo yaliyoko takribani kilometa nne na nusu chini cha usawa wa bahari.

Kusikia hivyo, Wachina walivutiwa kwa sababu abiria wengi wa ndege hiyo iliyopotea ni Wachina.

Ilimaanisha vingi kwamba baade alionekana kuyakwepa matamshi hayo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari tarehe 28 Aprili.

Wakati mwingine alikuwa na uhakika wa kukipata kifaa cha taarifa za ndege namba MH370, sasa Waziri Mkuu Abbott ameshangazwa na kuvunjwa moyo kwa sababu zoezi la utafutaji ndege umekwama

Wengi waliona kama ni kujichanganya mwenyewe:

Kwa nini Tony Abbott aliuambia ulimwengu mzima majuma machache yaliyopita kwamba alikuwa na uhakika jeshi la Australia limekipata kifaa cha taarifa za ndege MH370?

Abbott hadhani kabisa kwamba aliwaambia Wachina Australia imefanikiwa kuipata ndege ya MH370…lakini dunia nzima iliamini hayo kutokana na matamshi yake!

Akionekana kutokuogopa matatizo zaidi, Waziri Mkuu huyo alikwenda kwenye mkutano na waandishi wa habari:

Zoezi hili huenda likawa gumu kuliko ilivyowahi kutokea wakati wowote wa historia.

Hivi Abbott anajua chochote kuhusu fedheha? tafadhali onyesha kujali hisia za wanafamilia na acha kutangaza mambo usiyo na hakika nayo

Mambo yaliwaka kwenye mtandao wa Twita ambapo uzi unaohusiana na matamshi hayo ulianzishwa kumtuhumu kujaribu kuhamisha welekeo wa mjadala kufuatia kashfa mbaya kuhusu jamaa zake wa chama cha Liberal wanaokabiliwa na mashitaka mbele ya Tume Huru ya Ufisadi [ICAC] huko New South Wales. Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu juma lililopita kulifuatiwa na kuwajibika wa watu wengine zaidi kisiasa kuhusiana na utakatishaji wa fedha haramu.

Matamshi ya Abbott kuhusu ndege ya MH370 ni utani. Anataka kuhamisha welekeo wa mjadala wa kashfa ya fedha chafu inayorindima kwenye Tume Huru ya Ufisadi

Abbott alitangaza kwamba zoezi la kutafuta ndege kuwa ni utafutaji wa kihistoria. Ila (asisahau) zoezi la utafutaji linalofanywa na Tume Huru ya Ufisadi linaweza kulifunika zoezi hilo

Tony Abbott amejiandaa kuweka fedha zake mahali anakokujua yeye kiujanja, lakini baadhi wanadhani ni kupoteza wakati tu:

Siku 19 zilizopita maafisa wa Australia walitarajia kupata mabaki ya Ndege ya MH370 ndani ya siku chache. Sasa hivi imechukua miezi. Na zimetumia $milioni 60

Eneo la utafutaji kwa mara nyingine limepanuliwa, kwa kuwa dunia yote inatazama zoezi hilo katika hali ya kutokuamini:

Kwa hiyo Abbott kimsingi anasema hawajui lolote iliko ndege ya MH370

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.