Kikundi cha Boko Haram Chaendeleza Vitendo Vya Kigaidi Nchini Nigeria

Majuma ya hivi karibuni, kundi la Boko Haram limeendeleza kampeni yake ya kutekeleza mauaji kwa kuwachinja raia wa Nigeria wasio na hatia. Juma lililopita, kundi hili liliua wanafunzi zaidi ya 12  waliokuwa wakisafiri kwenda kufanya mtihani wa awali kwa ajili ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu katika jimbo la Borno. Kundi la Boko Haram pia linahusishwa na mlipuko wa bomu katika kituo cha mabasi uliotokea katika mji wa   Nyanya uliopo katika jiji la Abuja, mlipuko uliopelekea zaidi ya watu 70 kupoteza maisha.

Siku chache zilizopita, kundi hili  liliwateka nyara wasichana wanaokadiriwa kufikia 100   wa sekondari ya wasichana inayomilikiwa na serikali iliyopo Chibok, takribani kilometa 130 magharibi mwa Maiduguri kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Picha hapa chini inaonesha mlipuko mkubwa kuwahi kutokea katika historia ya nchi ya Nigeria. Boko Haram walidai kuhusika na ulipuaji wa bomu hilo:

Smoke and flames billow from the Police Headquarters car park Abuja, Nigeria. Photo by Ayemoba Godswill, copyright © Demotix (29?4?2013).

Moshi na moto vikivuma kutoka kwenye maegesho ya magari katika makao makuu ya polisi Abuja, Nigeria. Picha na Ayemoba Godswill, copyright © Demotix (29?4?2013).


Nchi ya Nigeria inapambana na  Boko Haram, kundi la kigaidi la kiislam linaloamini katika vita vya jihadi lililo na makazi yake kaskazini magharibi mwa Nigeria, kaskazini mwa Camerron na huko Niger, kundi lililokwishaua maelfu ya watu kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita. 

Wiki iliyopita, Boko Haram waliwafyatulia risasi  wanafunzi katika chuo cha kilimo kilichopo katika jimbo la Yobe,  waliwaua kwa risasi  makumi mawili ya wanafunzi waliokuwa na umri wa kati ya miaka 18 na 22 waliokuwa wamelala katika bweni lao. A Mfululizo wa mauaji yaliyotekelezwa kuanzia mwaka 2012 umefafanuliwa vizuri katika makala haya.

Watumiaji wengi wa mtandao nchini Nigeria wameshitushwa sana na ukatili huu wa hivi karibuni, wamemlaumu sana Rais Goodluck Jonathan  kwa kutokomeza hali ya utulivu nchini:

Wakati serikali kuu na maafisa wake wa usalama wakiwa ni mahiri kabisa wa kuandika hotuba nzuri za kuomboleza, kundi la BOKO HARAM linaendelea tuu kujiimarisha.

Wengine wanafikiri kwamba Rais hajaweza kufanya kile alichopaswa kukifanya: 

Boko Haram wanatekeleza mauaji kana kwamba wanarudisha fadhila na Rais anaendelea tuu na hotuba zake za kampeni zisizo na maana yoyote. Kutokuwajibika, uhuni usioelezeka!

@toluogunlesi alimmwagia sifa mshauri wa Masuala ya Ulinzi wa nchi Kanali Sambo Dasuki:

Ashukuriwe ndugu Dasuki kwani mwezi uliopita alizindua mkakati mzuri kabisa wa kukabiliana na magaidi. Hii ni kama tu uwasilishaji wa mawazo yake ungeweza kuokoa maisha.

Ni nani anayewawezesha kifedha Boko Haram, aliuliza Henry Bature Okelue:

Ni matumaini yangu kuwa, siku moja serikali itatujulisha ni nani anayewafadhili kifedha na kuratibu mikakati ya Boko Haram.

Photo released under Creative Commons by Wikipedia user Bohr.

Majimbo ya Nigeria ambayo Boko Haram huendeshea shughuli zao. Picha ilitumiwa kwa mamlaka ya Creative Commons na mtumiaji wa Wikipedia, Bohr.

Mtumiaji mmoja wa Twita alipendekeza wanachama wote wa Boko Haram wachinjwe:

Adhabu ya kifo ndio njia pekee ya kutatua tatizo hili. kila mwanachama wa Boko Haram hana budi kuuawa kwa kuchinjwa.

Ni hofu kubwa kwa mauaji na huzuni kuu kwa wahanga:

Nashindwa kuelewa ni kwa namna gani boko haram waliweza kuwateka nyara wasichana 200 wakiwa shuleni, hali hii bado inanitatiza.

Kitendo cha BokoHaram kuwateka nyara wasichana 100 girls ni cha kuchukiza mno. Goodluck Jonathan lazima sasa atangaze vita rasmi dhidi ya BokoHaram. Wafutiliwe mbali kabisa.

@onigabby1 anajiuliza kama Nigeria bado ipo:

Hivi Nigeria bado ni Nigeria? Au ni shirikisho la jamhuri ya boko haram. Ninawapa pole sana wahanga wote wa mlipuko wa bomu uliotokea.

Kuna njia muafaka ya kutatua tatizo hili?:

Kuna utatuzi wa ugaidi wa Boko haram?”Kwa kweli hakuna suluhisho, kinachowezekana ni kupunguza mfululizo wa mashambulizi yao.

@LovBwise awataka wanaharakati kuandamana:

Kuna utatuzi wa ugaidi wa Boko haram?”Kwa kweli hakuna suluhisho, kinachowezekana ni kupunguza mfululizo wa mashambulizi yao.

@opinion_river alionesha dhahiri kile anachokiamini: 

Rais Goodluck Jonathan siyo chanzo cha Boko-Haram. Kundi hili lilikuwepo hata kabla hajaingia madarakani. Lakini bado hajajituma vya kutosha katika kutokomeza kundi hili.

Baadhi ya watu waliwataka watu kusali:

Tafahali, tutumie muda wa dakika tano kuanzia saa 6 mchana hadi saa 6:05 mchana ili tusali sala hii:- Mungu uwasaidie wasichana wasio na msaada waliotekwa nyara na Boko Haram huko Borno

Wakati wengine wakihitaji mambo mengine zaidi kufanyika mbali na kusali: 

Wakati tunawaombea wale waliotekwa nyara na Boko Haram, mikakati lazima ipewe kipau mbele kutoka katika sehemu hiyo ya kusalia.

Mtumiaji @naitwt alikuwa na matumaini: 

Magaidi pamoja na wafadhili wao, waungaji mkono wa & wanaounga mkono uvurugaji wa amani, kudhalilisha & kuharibu – lakini watashindwa & sisi tutaendelea kudumu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.