Kampeni ya ‘Piga Kura ya Hapana’ Yawahamasisha Waafrika Kusini Kuvitelekeza Vyama Vikubwa

South Africa former

Waziri wa zamani wa usalama wa Afrika Kusini Ronnie Kasrils anaongoza kampeni ya kukipinga chama cha ANC. Picha imetolewa chini ya leseni ya Creative Commons na mtumiaji wa Flickr Russell Tribunal

Kikundi cha wanasiasa nchini Afrika Kusini kinaendesha kampeni ya kuwashinikiza wapiga kura kuvigomea vyama vikubwa siku ya uchaguzi itakapofika.

Waziri wa zamani wa usalama wa Afrika Kusini Ronnie Kasrils, kiongozi wa zamani wa Chama cha Kikomunisti cha Afrika Kusini Vishwas Satgar na aliyewahi kuwa naibu waziri wa Afya na Ulinzi Nozizwe Madlala-Routledge walizindua  kampeni yao ya “Piga kura ya hapana ya Vukani! Sidikwe! (Amkeni! Tumechoka!!)” jijini Johannesburg mnamo Aprili 15, 2014. Kampeni hiyo inawataka wapiga kura wa Afrika Kusini kuvipigia kura vyama vidogo wakati wa uchaguzi wa Mei 7 au basi waandike “Hapana” kwenye karatasi ya kura.

Kwa mujibu wa mtandao wa Business Day Live, kampeni hiyo imevutia vigogo wakubwa kutia saini kuunga mkono kampeni hiyo, kama vile mkurugenzi mkuu wa zamani wa mambo ya mazingira Horst Kleinschmidt, makamu mkuu wa chuo wa zamani wa Chuo Kikuu cha South Africa Barney Pityana, na mchora katuni maarufu aliyeshinda tuzo kadhaa Jonathan Shapiro.

Kampeni hiyo inafadhiliwa na mashirika kama vile Awethu Platform, Democratic Left Front na Democracy From Below.

Chama tawala cha African National Congress (ANC) knakabiliwa na mtihani mgumu kuwahi kukikabili chama hicho kwenye uchaguzi wa mwaka huu kufuatia kupanda kwa gharama za maisha, ukosefu wa kazi na kashfa za ufisadi. Wapinzani wakuu ni chama kikuu cha upinzani Democratic Alliance (DA) na Wapiganaji wa Uhuru wa Kielekroniki (EFF), na chama chenye msimamo mkali wa kushoto kilichoanzishw ana kiongozi wa zamani wa umoja wa vijana wa ANC Julius Malema.

Raia wa Afrika Kusini watumiao mtandao walionekana kugawanyika sana kuhusiana na kampeni hiyo kwenye mtandao wa Twita. Baadhi waliunga mkono jitihada hizo:

Sidikwe vukani. Piga kura ya hapana. Posti kwa mara nyingine kama tunataka kuilinda demokrasia yetu.

Hii Sidikiwe Vukani ni ujumbe uliowazi sana: “Haribu kura yako! Sawa, usiharibu, lakini basi mpigie yeyote isipokuwa ANC. Lakini pia sio DA, wala EFF!

Nikiwaunga mkono Madlala-Routledge ana Kasrils ninasema “Sidikiwe! Vukani!” “Tumechoshwa! Tuamke!”.

Hawa watu wa ANC wanadhani vijana wa Afrika Kusini ni vipofu. Hapana mmekosea. Tunayo macho mawili angavu na yanayoona sawia kila kitu kuhusu ANC

Wengine walipendekeza kwamba:

Kampeni ya “Piga kura ya hapana” inapotosha. Yapasw akuwa “Usikipigie Kura ANC”

Badala ya kutangaza sana kupiga kura ya hapana tuwe na uchaguzi wa kuwa na kisanduku cha ‘hakuna anayefaa’ kwenye karatasi ya kupigia kura, na kisha “hakuna chama” kinachofaa kutuongoza…

Wakati wengine walipinga kampeni hiyo, wakihoji mantiki na nia hasa ya kampeni hiyo:

Siafikiani na kampeni hii ya #KutokupigaKura, nina hakika mkakati wa ANC kuwafanya watu wasivipigie kura vyama vya upinzani! Sisi wa chama cha #EFF tunasema watu lazima wapige kura!

Tatizo langu kuhusu kampeni hii ya #Usipige Kura ni kwamba hakuna atakayehesabu kura hizi, sasa unawezaje kuweka alama kama hujapimwa?

Sielewi kabisa kampeni hii ya #UsipigeKUra! Kama huna imani na chama, pigia chama kingine. Fanya hivyo kukihafifisha chama ulichowahi kukiunga mkono

Kwa hiyo, kampeni ya ‘Sidikwe Vukani -Usipige Kura’ ilizinduliwa jana. Sitapoteza muda wangu kukipigia chama chochote kidogo, hata mara moja

Hiki kinachoitwa kampeni ya kuipinga ANC ya ‘Sidikiwe Vukani’ inayoongozw ana Khumalo inabaki kwa matusi ya kuzuia mapinduzi niliyowahi kuyaona tangu mwaka 1994.

Mtazamo wangu kuhusu kampeni ya Sidikiwe Vukani ni -badala ya kuharibu kura yako – uliza chama gani kinaheshimu katiba SASA!

Nadhani watu watatambua uongo…hakuna uhakika wowote kwenye kampeni ya Usipige Kura. Lazima tuhamasishe watu kupiga kura

Kwa hiyo wakati ninajisikia kutiwa moyo kuwa Kasrils hatimaye amefukuzwa, ninadhani imechukuwa muda mrefu sana na kampeni yake ya #HakunaKupigaKura haina maana yoyote
Kabla ya kuandaa kampeni hiyo, Ronnie Kasrils alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya ANC kwa miaka 20 na alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya chama cha Kikomunisti cha (SACP) kwa miaka 21. Alikuwa mjumbe mwanzilishi wa tawi la kijeshi la ANC la Umkontho we Sizwe.

Msemeaji wa ANC @ANC_KKhoza alimkabili mwanachama huyo wa zamani:

Ronnie Kasrils ana maumivu ya kujijenga upya. Amefikia kipindi cha kufubaa kisiasa

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.