Blogu ya Tunisia Yazindua Jukwaa la ‘Kuvujisha Taarifa Nyeti’

Blogu maarufu ya Nawaat iliyoshinda tuzo na inayofanya kazi kwa ushirikiano na blogu nyingine imezindua jukwaa lake la mijadala ya kisiasa litakalotumika kuibua masuala nyeti: Nawaat Leaks.

Jukwaa hilo salama lilizinduliwa kwa ushirikiano na GlobaLeaks, zana huru na inayoficha utambulisho wa mtumiaji. GlobaLeaks ilitangaza mradi wake mpya kwenye twiti ya Machi 27:

Tovuti ya kwanza ya kuvujisha taarifa kwenye nchi za Kiarabu imezaliwa na @nawaat kwa kutumia GlobaLeaks kwa lugha za Kiarabu na Kifaransa!

Nawaat Leaks Logo

Nembo ya Nawaat Leaks


Wale wanaotaka kutumia mtandao wa Nawaat Leaks ili kuvujisha taarifa nyeti, watahitaji kwanza kushusha zana ya kuficha utambuzi wa mtandao iitwayo Tor.

Mwanzilishi mwenza wa Nawaat, Sami Ben Gharbia anaeleza [ar] hatua za kuhakikisha usalama wa mtandaoni zilizochukuliwa kwa minajili ya kuwalinda watumiaji wa jukwa hilo :

قام فريق نواة بالتعاون مع مبادرة جلوبال ليكس بإنشاء صفحة خاصة تستخدم حزمة من التطبيقات و التقنيات المفتوحة المصدر التي تحمي مسربي الوثائق و الملفات السرية. هذه البرمجية تحمي المُسربين حتى من فريق نواة نفسه الذي لن يتعرف بفضل هذه التقنيات على هوية الأشخاص الذين سيقومون بعملية التسريب، لا عن طريق بريدهم الإلكتروني و لا عن طريق معرفهم الألكتروني و لا عن طريق إسمهم أو موقعهم الجغرافي.

و من أجل توفير حماية أكثر للمسربين سيعمل فريق نواة كعادته، قبل نشر أي وثيقة سرية مسربة، على فسخ كل البيانات الوصفية (Metadata) التي تزيد من إمكانية الكشف عن المصدر الإلكتروني للوثائق سواءا كانت ملفات صوتية، مقاطع فيديو، صور أو وثائق نصية.

Kwa kushirikiana na GlobaLeaks, timu ya Nawaat imeanzisha ukurasa maalumu unaotumia zana huru na teknolojia zinazowalinda wale wanaovujisha nyaraka na makarabrasha nyeti. Zana hii inawalinda “wavujishaji” wasifahamike na timu ya Nawaat yenyewe, inayoshukuru teknolojia hizi ambazo zitafanya isiwezekane kuwabaini wale wanaovujisha [tarifa] kupitia kwenye anuani zao za barua pepe, anuani zao za utambulisho wa kompyuta zao [IP], majina au maeneo yao ya Kijiografiia. Ili kuwalinda zaidi, timu ya Nawaat itakuwa ikifuta taarifa, kama ilivyo kawaida, taarifa zozote zinazoweza kuongeza uwezekano wa kufahamika chanzo cha taarifa katika namna tofauti: sauti, vipande vya video, picha au maandishi kabla ya kuchapisha nyaraka zozote

Mwaka 2011, serikali ya muda ya Tunisia ilipitisha amri 41 zinazomhakikishia yeyote upatikanaji wa nyaraka za kiutawala. Kwa vitendeo, hata hivyo, sheria haijaweza hata kukaribia utekelezaji. Kwenye tamko lililochapishwa Machi 27, ibara ya 19 iliikosoa serikali kwa kushindwa kutekeleza sheria hizo 41.

IBARA YA 19 “inabaisha wasiwasi uliopo kwamba hatua zilizopo zimetengenezwa kuhakikisha kuwa uwazi wa serikali hautekelezeki kwa ufanisi” shirika hilo lilisema.

Ben Gharbia anatoa maoni [ar] kuhusu kutokuwepo kwa utekelezaji stahili wa sheria hii:

بالرغم من المرسوم عدد 41 لسنة 2011 الذي يضمن، نظريا، حق المواطن في النفاذ إلى الوثائق الإدارية للمنشئات العمومية، و بالرغم من كثرة الحديث عن مقاومة الفساد و محاسبة الفاسدين و ضرورة تأسيس حوكمة رشيدة قائمة على الشفافية، إلا إننا لم ننعم بعد لا بحق النفاذ إلى المعلومة و لا بمقاومة جادة للفساد. بل على العكس، رأينا كيف يُحاكم و يتبع عدليا كل من حاول كشف المستور من فساد و محابات واستغلال للنفوذ و غيرها من المظاهر التي لا تزال تنخر عوالم السياسة و الإدارة و الأعمال

Pamoja na sheria 41 za mwaka 2011, ambayo kinadharia inawahakikishia raia haki ya kupata taarifa za kiserikali kutoka kwenye taasisi za umma na pamoja na mazungumzo mengi kuhusu kupambana na ufisadi na kuiwajibisha serikali na hitaji la kuanzisha utawala bora ulio wazi [sera], bado hatujaweza kufaidi haki ya kupata taarifa hizo na kushuhudia vita vya kweli kweli vya kupambana na ufisadi. Lakini, kwa upande mwingine, wameshuhudia namna wale wanaotafuta kuibua taarifa za ufisadi uliojificha, upendeleo wa kindugu, matumizi mabaya ya madaraka na namna nyingine zinazotishia na kuathiri siasa za dunia, utawala na biashara

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.