Habari kutoka 21 Aprili 2014
M-Misri Atumia Mtandao wa YouTube Kupinga Kutumikia Jeshi kwa Lazima
Mwanaharakati wa Misri ametumia mtandao wa YouTube kuelezea anavyopinga utaratibu wa kulitumikia jeshi kwa lazima kwa raia wenye umri wa miaka kati ya 18 na 30. Katika barua pepe aliyoituma kwa Global Voices mtandaoni, Adam anaandika: Mimi ni Mmisri mwangalifu ninayepinga kwa nguvu zote utaratibu wa kulitumikia Jeshi la Misri...
Serikali Mpya ya Waziri Mkuu Roger Kolo Yatangazwa Nchini Madagaska
Mtandao wa Tananews nchini Madagascar umechapisha orodha kamili ya mawaziri 31 wa serikali mpya ya Madagaska [fr]. Mitsangana Madagascar anasema kwamba orodha hiyo ina wanawake 6 na kuwa mawaziri 7 walikuwa kwenye baraza[fr] la serikali iliyopita ya mpito. Waziri mkuu wa zamani Beriziky aliitakia serikali kila la heri kwenye mtandao...