Mwandishi, Mpiga picha na mwanablogu Meg at Life in Lanka anaripoti kuwa kwenye sehemu za vijini nchini Sri Lanka baadhi ya wanawake hawana kauli kuhusu aina ya mpango wa uzazi wanaoutaka.
Waume zao hawatumii kondomu na wanapenda wake zao watumie mbinu nyingine za kupanga uzazi; kwa hiyo njia rahisi inayopatikana kirahisi na yenye ufanisi ya kutumia kondomu haipendwi na wanaume, hiyo ikifanya suala la kujikinga na mimba zisizotarajiwa kuwa ni wajibu wa mwanamke.
Kwa sababu ya ukweli kuwa madawa ya kupanga uzazi mara nyingi yana madhara kwa wanawake, mateso hayo huwa hayaishi.