- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Video: Usambazaji Vyakula katika Kambi ya Yarmouk-Syria

Mada za Habari: Syria, Chakula, Haki za Binadamu, Maandamano, Majanga, Mwitikio wa Kihisani, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vita na Migogoro, Vyombo na Uandishi wa Habari, Wakimbizi, Wanawake na Jinsia

Shirika la habari la FAJER [1] liliweka mtandaoni video ya kambi ya wakimbizi ya Yarmouk [2] mjini Damascus wakati wa kupokea mgawo wa chakula cha kuwalisha wakazi 18,000 wa kambi waliobaki, ambao wamelazimishwa kula wanyama waliopotea ili kuokoa maisha yao wakati huu ambapo kuna uhaba mkubwa wa chakula.

Video ni ya tarehe 30 Desemba 2013