VIDEO: “Nyumba ya Kusubiri” kwa Wajawazito Nchini Peru

Ripoti kwenye video iliyowekwa kwa hisani ya Oscar Durand na Elie Gardner mahususi kwa ajili ya nchi zinazoendelea;ilionekana kwenye tovuti wa PRI.org mnamo Februari 23, 2014 na kuchapishwa kama sehemu ya makubaliano ya kugawana maudhui.

Katika maeneo ya vijijini nchini Peru, wanawake wanahamasishwa kutumia juma la mwisho wa ujauzito katika sehemu maalumu ambayo hutoa faraja na huduma. Lakini hata hivyo wakati huo wa kusubiria uzazi unabakia kuwa mgumu.

Ili kuzuia wanawake kutokujifungua nyumbani, hali inayoweza kusababisha hatari kubwa ya kifo, Peru imeanzisha mtandao wa “nyumba za kusubiri” kwa wazazi. Huduma zilizo katika makazi haya ni mahususi kuhudumia wanawake wanaotokea katika maeneo ya vijijini wakati wa juma lao la mwisho la ujauzito, ili waweze kujifungua kwa msaada wa wakunga wenye ujuzi. Ana Maria Bolege, 21, amefika katika nyumba ya kusubiri katika mji wa Andean ya Ayacucho, masaa matatu kwenye njia ya barabara kutoka nyumbani kwake.

Makala haya ni sehemu ya mpango wa Mwezi wa Tisa unaoratibiwa na PRI, unaofuatilia safari za uzazi mpaka wakati wa kujifungua, katika tamaduni mbalimbali na mabara tofauti. Jiunge na kikundi chaMwezi wa Tisa katika mtandao wa Facebook kupata habari za kujifungua za mahali unapoishi.. kupitia alama ashiria kwenye mtandao wa twita #ninthmonth

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.