Machi 5, Umoja wa Shirika la Ulaya kwa Haki za Msingi (FRA) ilichapisha matokeo ya utafiti juu ya unyanyasaji dhidi ya wanawake[pdf], uliokuwa wa kina zaidi na wa aina yake kuwahi kufanywa. Ukiwa umefanywa kwa wakati mmoja katika kanda nzima, ni mara ya kwanza takwimu za ulinganisho zimemeza kupatikana katika nchi kuhusu aina ya vurugu ambazo wanawake wanakabiliwa nazo katika familia zao, kazini, katika umma na kwenye mtandao pamoja na athari inayo katika maisha yao na njia ambayo waathirika hukabiliana na uchokozi.
Ripoti hiyo imejikita katika mahojiano ya moja kwa moja na wakazi 42,000 wa kike wa Umoja wa Ulaya wenye umri wa miaka kati ya 18-74, idadi ambayo ni kubwa. Kwa mujibu wa moja ya video zilizotolewa sambamba na ripoti hiyo, “matokeo yanaonyesha kiwango cha unyanyasaji dhidi ya wanawake katika Umoja wa Ulaya ni kikubwa, na hakiwezi kupuuzwa tu.” Kwa maneno ya Mkurugenzi wa FRA Morten Kjaerum:
La enormidad del problema prueba que la violencia contra las mujeres no afecta solo a unas pocas: tiene impacto en la sociedad todos los días. Por tanto, políticos, sociedad civil y trabajadores de primera línea tienen que evaluar medidas que traten cualquier forma de violencia contra la mujer, donde sea que se produzca.
Ukubwa wa tatizo ni uthibitisho kwamba unyanyasaji dhidi ya wanawake si tu unaathiri wanawake wachache tu – ni madhara kwa jamii kila siku. Kwa hiyo, watunga sera, vyama vya kiraia na wafanyakazi walio mstari wa mbele wanahitaji kufanyiwa tathmini ya hatua za kukabiliana na aina zote za ukatili dhidi ya wanawake hakuna jambo bila kujali ambapo inafanyika. [sic] [sic]
Miongoni mwa mahitimisho ya utafiti huo ni pamoja na:
- 33% ya wanawake wamekuwa wakikabiliana na udhalilishaji na / au unyanyasaji wa kijinsia tangu umri wa miaka 15, wakati asilimia 5 wamebakwa.
- 55% ya wanawake huteseka kwa aina fulani ya unyanyasaji wa kijinsia (mfano kupigwa busu bila hiari yao, kukumbatiwa au kuguswa) tangu wakiwa na umri wa miaka 15.
- 75% ya wanawake katika ajira ya kiwango cha juu au wenye ujuzi wa juu wamekabiliwa na matukio ya unyanyasaji wa kijinsia wakati fulani katika maisha yao.
- 11% ya wanawake wamewahi kukumbana na unyanyasaji wa kijinsia kupitia barua pepe au ujumbe mfupi (SMS).
- 67% hawakuripoti tukio kubwa zaidi la udhalilishaji waliofanyiwa na wapenzi wao kwa polisi au mashirika mengine.
Jambo la kushangaza ni nchi zenye asilimia kubwa ya waathirika wa unyanyasaji dhidi ya wanawake ni zile za eneo la kaskazini mwa Ulaya: Denmark (52%), Finland (47%) na Sweden (46%), wakati Hungary (21%), Austria (20%) na Poland (19%) wana viwango vya chini sana. Hispania, katika 22%, ni vizuri chini ya wastani:
Inaonekana wazi kwamba nchi za Scandinavia, ambazo zina viwango vya juu vya usawa wa kijinsia, ndizo zenye viwango vya juu dhidi ya unyanyasaji wa wanawake. Blanca Tapia, msemaji wa FRA,, anaelezea katika gazeti la El Diario [es] mgongano huu ulio wazi:
En países como Finlandia, Dinamarca, Suecia o Francia es más aceptable culturalmente hablar de violencia de género y, por lo tanto, las mujeres la declaran más. Las mujeres de los países nórdicos tienen mucha conciencia de género, saben que son iguales en derechos a los hombres y tienen claro que no tienen que aguantar ciertas cosas. No pasan ni una.
Katika nchi kama Finland, Denmark, Sweden au Ufaransa, imekuwa ni utamaduni unakubalika kuwa na majadiliano juu ya unyanyasaji dhidi ya wanawake, hivyo wanawake wana uwezekano wa kuyakemea. Wanawake katika nchi za Ulaya Kaskazini wana uelewa mkubwa wa kijinsia; wanajua wana haki sawa kama wanaume na ni wazi kwao kwamba kuna mambo fulani hawawapaswi kukubaliana nayo. Hawawezi kuruhusu mambo fulani kuwapata.
Ripoti imezua utata kati ya Wazungu. Wengi wanatia shaka ukweli wa idadi na kuzua swali ni nini hasa kuchukuliwa kama kushambuliwa. Mtumiaji DENUNCIAR aliacha maoni yafuatayo katika tovuti ya [es]:diario 20 minutos [es]:
ya sabemos como hacen las encuestas estas feministas, si se pelean por el mando de la tele se considera violencia machista
nada nuevo bajo el sol
otra noticia para manipular nuestras mentes en el siglo dorado del feminazismo
Sisi tayari tunajua jinsi tafiti hizi za masuala ya kijinsia zinavyofanya kazi, mkibishana kidogo na mpenzi wako kuhusu “rimoti” ya televisheni hiyo inatosha kuchukuliwa kuwa udhalilishaji wa kijinsia
Hakuna kitu kipya chini ya jua
Hizi ni habari nyingine zilizotengenezwa kuendesha akili zetu wakati huu wa kukomaa kwa wapigania haki za akina mama
Katika gazeti la Público, chochialimmoomuelte alitoa maoni:
¿¿Una de cada cinco mujeres no sabe que si la violan tiene que ir a la policía??
¿¿Decir “no te quiero” a alguien es violencia machista??
¿¿Los abrazos son acoso??
¿¿ La “violencia contra las mujeres” se da “todos los días en todas partes”??
Desde luego, cada vez os cuesta más justificar las subvenciones al chiringuito feminazi.
Las mujeres inteligentes deberían indignarse ante esta basura que se publica en las que se las trata como si fueran imbéciles
Mmoja kati ya kila wanawake watano hajui kwamba anapaswa kutoa taarifa za ubakaji kwa polisi??
Kusema “mimi sikupendi” ni udhalilishaji??
Kumkumbatia mtu ni unyanyasaji wa kijinsia??
“Udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake “hutokea” kila mahali kila siku”??
Bila shaka, inakuwa vigumu zaidi kuhalalisha kutoa ruzuku inayotokana na kodi zetu kwa mashirika haya yanayojifanya kupigania haki za wanawake.
Wanawake wenye akili lazima wawe na mashaka na upuuzi huu uliochapishwa ili kuwafanya waonekane ni punguani.
Madame X aliwajibu wenye mashaka na ripoti hiyo kwenye tovuti hiyo:
Por supuesto que un piropo grosero es una agresión. Es humillante que te digan una grosería y la humillación es una forma de maltrato. Cualquier tío se ofendería si otro le dice una grosería a su novia, a su madre o a su hermana, ¿o me lo vais a negar? Entonces si eso os ofende o molesta cuando va dirigido a una mujer de vuestro entorno afectivo, ¿cómo algunos tenéis la cara dura de cuestionar que eso sea una agresión a la afectada?
Bila shaka maoni ghafi ni aina ya uchokozi. Ni kudhalilisha kuwa na kitu ghafi kusemwa kwako wewe, na udhalilishaji ni aina ya kutendewa vibaya. Mtu yoyote atakuwa na mashaka kama mwingine angesema jambo linalochukiza kwa mpenzi wao, mama au dada-wewe waweza kupinga hayo? Hivyo kama umechukizwa au unasumbuliwa inaelekezwa kwa mwanamke unayemjali, jinsi gani baadhi yenu mna ujasiri kuuliza swali kama mwanamke anahisi kunyanyaswa?
Kwenye mtandao wa Twita; Lau alichapisha picha inayoelezea kwa undani aina mbalimbali za unyanyasaji wa jinsia dhidi ya wanawake:
Y no sólo me refiero a que nos revienten la cara con un guantazo o nos violen. La violencia machista tiene pilares pic.twitter.com/SKNIcY0L9r
— Lau (@mcmihail) March 5, 2014
Na mimi simaanishi tu wale wa kwetu ambao hupigwa kofi kwa uso au kubakwa. Udhalilishaji wa macho una mfumo.
[Piramidi inaeleza maendeleo kutokana na aina ya hila kama vile matangazo ya kijinsia na kupuuza wanawake na aina wazi zaidi kama vile matusi, unyanyasaji na hata mauaji.]]
Don Mitxel Erregea anazua maswali kuhusu jukumu la dini:
me pregunto si la violencia machista tendrá algo que ver con el fomento de religiones que asocian la mujer al Mal.
— Don Mitxel Erregea (@DonMitxel666) March 6, 2014
Nashangaa kama udhalilishaji wa kutumia macho wanafanya kitu kuhamasisha dini ambazo hujiunga na wanawake wabaya.
Nchini Hispania, kupunguzwa kuliotolewa na serikali ya sasa kunaathiri programu za umma zinazolinda wanawake [es]:
[La Ley de Tasas] elimina la falta por “vejaciones injustas” que suele ser el primer paso en los casos de maltrato, se sugiere la mediación en los casos de violencia de género. Esto pondría en riesgo a la víctima y se solicita que la condena del agresor sea una multa
[Sheria kuhusu ada ya mahakama] hupunguza kosa la “kutotendewa haki” ambalo ni kawaida hatua ya kwanza katika kesi ya matumizi mabaya; upatanishi unahitajika katika kesi za unyanyasaji dhidi ya wanawake. Hii itakuwa kuweka waathirika katika hali ya hatari na inataka kulazimisha tu faini kwa mchokozi.
Nchini Hispania, waathirika 48 wa unyanyasaji dhidi ya wanawake walikufa katika mwaka wa 2013. Hadi sasa katika mwaka wa 2014, wanawake 14 wameuawa na wapenzi wao.