- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Ufisadi Nchini Nepal: Umeanza Kuwa Tabia Inayokubalika Kijamii?

Mada za Habari: Asia ya Kusini, Nepali, Maandamano, Maendeleo, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala

Watu wana hasira na wamechoka, na mashirika ya habari mara nyingi huchapisha habari kuhusu uhusiano kati ya viongozi wa kisiasa na wezi wa mali za umma lakini hakuna anayezungumzia kuingia mtaani kuandamana kupinga ufisadi -hali isiyotarajiwa kwenye nchi ambayo watu hugomea kila kisichokwenda sawa

Siromani Dhungana [1] anaandika uchambuzi kwenye blogu ya United We Blog! akieleza mwenendo wa hali ya mambo nchini Nepal kwa kuonyesha ufisadi namna ufisadi unavyoanza kuwa sehemu ya maisha na kukubalika.