- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Teknolojia ya Kiafrika: Mradi wa TechAfrique Watathmini Hatua Iliyofikiwa

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Kenya, Maendeleo, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia

 Le continent africain apparaît comme la nouvelle frontière mondiale du développement numérique. Ce développement provoque une nouvelle impulsion entrepreneuriale en Afrique, et notamment en Afrique francophone. Mais ce potentiel reste très largement méconnu en Europe ainsi qu'en France. 

Bara la Afrika linaonekana kuwa kiongozi mpya wa dunia katika maendeleo ya kidijitali. Maendeleo haya yamesababisha kukua kwa ujasiria mali mpya barani Afrika, hususani kwenye nchi zizungumzao Kifaransa. Lakini uwezo huu unabaki kuwa siri isiyofahamika huko Ulaya na Ufaransa.

Kubadili hali hii, Samiri, mwandishi wa blogu ya  Startup BRICS [1] [fr] ilijikita kwenye miradi mipya katika nchi zinazoendelea, aliandaa safari za kiuchunguzi zilizoitwa  Mradi wa TechAfrique [2] ili kugundua na kuorodhesha miradi iliyopo na ile mipa, miradi ya Fablabs, na kwenye maeneo mengine yanayofanana na hayo katika ubunifu wa kiteknolojia katika nchi zizungumzao Kifaransa pamoja na Kenya.