Tangazo la Shindano la Kupata Ufadhili wa Rising Voices 2014

Je, unalo wazo la mradi wa kuisaidia jamii inayokuzunguka iweze kutumia mitandao ya kijamii kuandika habari zao? Je, unahitaji ufadhili na msaada ili kulifanya wazo hilo litekelezeke? Je, unataka kuwa sehemu ya mtandao unaosaidia kuziba pengo la ushiriki wa kidigitali?

Kama jibu lako ni “ndio” kwa maswali yote matatu, basi tunakukaribisha kushiriki kwenye Shindano la Kupata Ufadhili la Rising Voices 2014 .

RisingVoices-microgrants2014-600

UFADHILI

Rising Voices inawasaidia watu wanaoshirikisha jamii zao elimu na ujuzi kuhusu uandishi wa kiraia kwa njia za kidigitali na ushiriki wa kiraia. Tangu mwaka 2007, tumesaidia miradi midogo ya uandishi wa kiraia ipatayo 40 kwa kutoa fedha na utaalamu na vile vile kuwakaribisha kwenye familia ya Global Voices.

Miradi hii imewasaidia viongozi wa maeneo mengi kutambulisha “sauti” mpya na zisizosikika kwenye mijadala ya kidunia mtandaoni, ili kuangazia masuala ambayo ni ya muhimu kwa jamii zao.

Kwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita ya kuendesha mashindano ya namna hii, tumeona namna uelewa wa zana za kidijitali na mawasiliano zilivyoenea kwa kasi. Tumepokea maelfu ya maombi kutoka kwenye nchi zaidi ya 100. Kwakulitambua hili, tunaongeza idadi ya ufadhili tutakaoutoa mwaka huu, hata kama itapungua kidogo kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Mwaka 2014, tutatoa ufadhili wa kati ya Dola za Marekani 2,000-2,500 kwa miradi 10 yenye mawazo thabiti na bayana jinsi itakavyoelimisha na kusaidia jamii zao. Wanufaika wapya wataingia moja kwa moja kwenye mtandao wa Rising Voices na wataonekana kwenye mtandao wa Global Voices.

MWONGOZO

Rising Voices inatafuta maombi [proposals] ambayo yatawiana na maono yetu ya kutumia uandishi wa kiraia kama zana za uwezeshaji wa watu, uelewa baina ya watu na mabadiliko ya kijamii.

Tafadhali tazama orodha ya wanufaika wa sasa na waliopita kama mfano wa miradi iliyowahi kufadhiliwa siku za nyuma.

Tunatafuta miradi ambayo:

1. Inawahusisha wanajamii wa maeneo kadhaa ambao “hawawakilishiwi ipasavyo” mtandaoni, ama kwa idadi, lugha au kijiografia. Tunatafuta kuwasaidia viongozi ambao wao wenyewe wanaishi kwenye jamii hizi na kujua namna na kwa nini uandishi wa kijamii ungeweza kuzisaidia jamii zao. Kama mwombaji si mmoja wa wanajamii wake, wakazi wa maeneo yanayolengwa au wanajamii lazima awe sehemu ya kutengeneza na kuutekeleza mradi.

2. Kutoa mafunzo, maelekezo na uongozi. Tunataka vingozi wa miradi wenye juhudi ya kushirikisha wengine maarifa na ujuzi wao. Kwa kutumia mafunzo rahisi katika mbinu za uandishi wa kiraia, washiriki watajisikia kuandaliwa na hivyo kuwa na ujasiri kwa kutumia zana. Msaada endelevu ni suala la lazima katika kutengeneza jamii ya uandishi wa kidijitali wenye faida.

3. Kusimulia habari za kidijitali kuhusu masuala muhimu kwa jamii. Baada ya washiriki katika warsha za mafunzo watakuwa tayari kushiriki sauti zao kwa dunia. Tunatafuta habari ambazo zitatupa uelewa wa jamii husika, mabadilko yao au mafanikio yao, zinazosimuliwa kwa mtazamo pekee wa kibinafsi.

4.Kutumia zana huru za uandishi wa kiraia zinazopatikana vya kutosha na majukwaa ya mitandao ya kijami. Hii inaweza kujumuisha blogu, na mitandao kingine ya kijamii kama Twita, zana huru kama Audacity kwa ajili ya kuhariri sauti, Audioboo, or Radioteca. Tovuti za video kama YouTube na Vimeo, au zana za ramani kama OpenStreetMaps. Unaweza pia kufikiri kutumia mitandao ya kijamii kama Facebook kusambaza maudhui yako.

Tunakuhamasisha kuwa mbunifu na mwenye ari, lakini ukiwa na uhalisia unapoandika maombi yako. Tazama Maswali Yanayoulizwa Mara nyingi kwa taarifa zaidi.

Ili kuomba, tafadhali tembelea ukurasa ulioandikwa “Submit a Proposal” [tuma pendekezo lako], ambapo utakuta maswali madogo yatakayokusaidia kuchambua mpango wa mradi wako. Tunashauri uwe na majibu mafupi na ya bayana (kukiwa na idadi ya herufi zisizotakiwa kuzidi) kukusaidia kuweka sawa mawazo yako kuwa kile kinachohitajika zaidi.

MCHAKATO WAZI

Tunakushauri kusambaza maombi haya kweeye mitandao na majukwaa ya wazi. Matumaini yetu ni kwamba jamii zinazofanya kazi kwa karibu au kwa masuala yanayofanana, wanavyowasiliana na kushirikiana.

2014 Rising Voices Microgrant Platform

Jukwaa la Ufadhili wa Rising Voices 2014

Maombi ya mwaka jana bado yanapatikana mtandaoni na mengi yana njia za kukuwezesha kuwasiliana na waombaji kupitia mitandao ya Twita au Facebook. Tafadhali pitia maombi ambayo yanaweza kuwa yanatoka kwenye eneo lako au yanaangalia masuala yanayofanana na jaribu kuchunguza kama kushirikiana kunawezekana.

Tutatoa upendeleo maalum kwa maombo ambayo yataonesha jitihada za kujenga ushirikiano na waombaji wengine. Kuna swali kwenye fomu ya maombi linalokutaka ueleze ushirikiano wako, tafadhali weka taarifa hizo.

Kama hutaweza kushirikishana na wengine taarifa za maombi yako kiuwazi kwa sababu za kiusalama, una uchaguzi wa kutuma kwa siri.

TARATIBU ZA MAOMBI

Shindano hili litafuata utaratibu wa muda kama ifuatavyo:

Kufungua maombi:Jumatano, Machi 12, 2014

Waombaji watume maombi yao ya awali kwa kupitia jukwaa la mtandaoni kwa lugha ya kiingereza (tafadhali kigezo hiki ni kwa sababu kamati ya kupitia mambo hayo inatumia lugha moja rasmi). Baada ya maombi yako kutumwa mtandaoni, tunakaribisha waombaji kutoa taarifa za maombi yao kwenye mitandao yao, ili kupata maoni na kupata mawazo zaidi kutoka kwa wengine.

Maombi yote yatapitiwa na kamati ya watu kutoka kwenye familia ya Global Voices, inayojumuisha wanufaika wa zamani wa ufadhili mdogo.

Tarehe ya mwisho kutuma maombi: Jumatano, Aprili 9, 2014 saa 5:59 GMT

Washindi watatangazwa: Jumatano, Mei 7, 2014 (tarehe inaweza kubadilika kutegemeana na idadi ya maombi yatakayokuwa yanapitiwa).

Tafadhali jisikie huru kuuliza maswali kwa kuacha maomni au kutuma barua pepe kupitia Fomu yetu ya Mawasiliano.

Kila la Heri!

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.