Polisi Wawatazama Raia Wakiandamana Nchini Macedonia

Kama ilivyokuwa imepangwa,  saa 5:55 za asubuhi juu ya alama ,  Maandamano yaliyojulikana kama “6 kasoro (dakika) 5 ” dhidi ya Umasikini yalianzia kwenye bunge la Macedonia katika jiji la Skopje, mnamo tarehe 1 Machi, 2014. Photo/a> and picha za mnato na video zilizopigwa kwneye maandamano hayo zinaonyesha kuwa kadri ya watu 1000 walishiriki maandamano hayo huku kukiwa na idadi kubwa ya polisi waliokuwa wakilinda usalama kwenye njia ya waandamanaji hao. Tukio hilo liliishia kwenye “Tamasha la Utu” lilikuwa la wazi kwenye viwanja vya  Jadran Square.

Macedonia, nchi iliyo kwenye orodha ya nchi masikini kabisa barani Ulaya, kila mwananchi mmoja kati ya watatu anaishi chini ya mstari wa umasikini [pdf].

March against Poverty in Skopje, March 1, 2014. Photo F.S. CC-BY.

Maandamano ya Kupinga Umasikini jijini Skopje. Picha ya mwandishi wa makala haya tarehe 1 Machi, 2014. CC-BY- 2.0

Waandaaji wa tukio hilo, Septemba 8 na Jukwaa la Macedonia Kupinga Umasikini, wanadai mabadiliko katika sheria za ustawi wa jamii ili kuwapatia kipato cha kumudu maisha raia wa Macedonia waliomasikini kabisa. Tukio hilo lilifanyika kwa amani, ukiacha tukio moja tu ambapo afisa wa Polisi alimbughudhi mwandishi mmoja na mwandamanaji mwingine mmoja.  Mwanaharakati Petrit Saracini aliandika [mk] kwenye mtandao wa Facebook:

Dobro pomina marsot i koncertot protiv siromastijata, bez incidentite koi gi najavuvaa mediumite na vlasta. Osven eden moment, koga, koj drug, ako ne policijata, povotrno prekardasi, i legitimirase snimatel, a koga direktorkata na Helsinski gi prasala sto pravat, grubo ja otturnale. Pred lugje i kameri. Ic ne im cue. Na edvaj ni 1000 lugje izvadija 1000 dzandari. Nazdravje neka im se dnevnicite. I tie gi plakjame nie.

Maandamano hayo pamoja na tamasha la kupinga umasikini vyote vilikwenda vizuri, bila kutokea matikio yaliyokuwa yametabiriwa na vyombo vya habari vinavyoishabikia serikali. Isipokuwa kwa wakati mmoja, ambapo, nani mwingine ila polisi, aliomba kupata kitambulisho cha mpiga picha. Mkurugenzi wa Kamati ya Helsinki alipouliza kile walichokuwa wakikifanya, alisukumwa kwa nguvu na kuanguka, mbele ya watu na mbele ya kamera. Hawakujali. Kwa sababu labda watu chini ya 1000 walikuwa wakizungukwa na maafisa 1000 wa polisi waliokuwa na silaha. Tunawatakia matumizi mema ya fedha walizolipwa kwa kazi ya ziada. Tunawalipa hata hivyo.

Mkurugenzi wa  Kamati ya Helsinki nchini Macedonia , shirika la haki za binadamu, Uranija Pirovska alisema [mk] kwamba alikusudia kufungua malalamiko dhidi ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kutumia kipande cha video kilichochukuliwa kwenye tukio hilo, na kwa kutumia ushahidi wa watu waliokuwepo eneo hilo.

Mwezi Septemba 2013, kituo cha televisheni cha binfasi Nova TV kilitangaza na kuchambua [mk] tukio kama hilo, ambapo polizi walimlazimisha mpiga picha wao kufuta kipande cha video kilichokuw akinaonyesha ukatili wa polisi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wanajaribu kulinda eneo la bustani ya wazi inayotambulisha jiji la Skopje dhidi ya uharibifu. Mpaka leo, hakuna hatua yoyote imechukuliwa dhidi ya waliohusika na tukio hilo.

In front of the Government the protesters were met by police cordon and a cordon of ancient statues. The Government is turning the modernist facade into so-called 'baroque' style characteristic of Skopje 2014, at initial cost of EUR 9 Million. Photo: F.S. CC-BY.

Mbele ya majengo ya serikali waandamanaji walikutana na msusuru wa polisi na msusuru wa sanamu za kale -kazi za sanaa za kihistoria- zilizowekwa pale tangu mwaka 2007. Chini ya  Mradi wa Skopje 2014, serikali inakusudia kubadilisha eneo hilo la kisasa kuwa madhari ya mtindo wa kigen kwa kutumia euro milioni 9. Picha imepigwa na mwandishi wa makala haya. CC-BY.

maandamano hayo yaliandaliwa na kutangazwa kupitia  Ukurasa wa Matukio katika mtandao wa facebook, a blogu na kwenye mtandao wa Twita kwa kutumia alama habari  #5до12 and #5do12 .

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.