- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Namna Tabia ya Kula Hotelini Inavyoathiri Utamaduni wa Kula Mtaani Indonesia

Mada za Habari: Uandishi wa Habari za Kiraia

Ismanto kutoka Yogyakarta nchini Indonesia anabainisha [1] namna mtindo mpya wa kimagharibi wa kula mikahawani unapunguza tabia ya kula “vyakula vya kufunikwa na plastiki” inayofahamika kama ‘angkringan':

… vyakula vya angkringan vimepungua. Wanafunzi hawazitumii tena, wakifurahia kulipia vyakula ghali bei iliyo mara mbili zaidi, kunywa na kujumuika na watu katika mtindo wa mikahawa. Kama wanafikiria chakula cha angkringan, basi itakuwa ni cha tofauti, chenye hadhi ya chini kinachopondwa na watu wasio na fedha, tabaka la masikini na watu wa kizamani. Na mara nyingi panakuwa hakuna hali kujiona fahari kwa wanafunzi kwenye ‘kampani’ yake.