Machi 16, 2014 inakuwa ndiyo siku ya 1,000 ya kufungwa kwa mwandishi wa Ethiopia Reeyot Alemu. Anatumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya kutiwa hatiani katika mashitaka ya ugaidi mwezi Januari 2012.
Reeyot, mwalimu wa Kiingereza, alipokea Tuzo ya UNESCO-Guillermo Cano ya Uhuru wa Habari Duniani, Tuzo ya Hellman/Hammett, na Tuzo ya Mwandishi Jasiri ya Mfuko wa Habari wa Kimataifa kwa Wanawake.
Kwa mujibu wa Kamati ya Kulinda Waandishi (CPJ), serikali ya Ethiopia imehukumu waandishi na wanablogu huru wapatao 11 ikiwa ni pamoja na Reeyot na Eskinder Nega chini ya sheria ya kupambana na ugaidi tagu mwaka 2011. Katika waliofungwa ni pamoja waandishi wawili wa Sweden wanaotumikia kifungo cha miaka 11 kwa kudaiwa kukisaidia kikundi cha Waasi wa Kabila cha Kisomali.
Katika posti hii ya blogu, mwanablogu BefeQadu Z Hailu alielezea hatari ya kufungwa inawakabili waandishi wa habari wa Ethiopia:
Kama lengo la kifungo ni kuwasahihisha waliohukumiwa, basi kusisitiza kusoma na elimu yapaswa kuwa ni nyenzo ya kufikia lengo hilo. Katika gereza la Kality vyote hivyo vinaruhusiwa lakini si kirahisi kwa waandishi hawa na wengine waliohukumiwa kwa makosa yanayohusishwa na “ugaidi”.
Wafungwa hawa hawaruhusiwi kupata vitabu. Eskinder anasema, “Hususani vitabu vile vyenye vichwa vya habari vinavyounganisha maneno ‘Ethiopia’ na ‘Historia’ haviruhisiwi”. Hali ni hiyo hiyo kwenye gereza aliko Reeyot Alemu na wengine kama Wubshet Taye, Bekele Gerba, na kadhalika.
Magazeti na majarida huru yanayochapishwa nchini humo hayaruhusiwi gerezani; Eskinder alinieleza zaidi kwamba hata cheneli za TV kama BBC na Aljazeera haziruhusiwi kutazamwa kwenye maeneo ambayo yeye na wenzake wamefugwa.
Reeyot Alemu, baada ya mapambano magumu na utawala wa gereza na baada ya vyombo vya habari kufunua ukweli huo, sasa anaruhusiwa kupata masomo kwa njia ya masafa. Ila, bado ni vigumu kwake kupata vitabu vya ziada ukiacha vile anavyotumiwa moja kwa moja kutoka chuoni.
Watumiaji wa mtandao wa twita walituma twiti kwa kutumia alama habari #ReeyotAlemu kuonyesha mshikamano wao kwa mwandishi huyo aliyefungwa. Hapa chini ni baadhi ya twiti zilizotumwa:
Hope the world cares about her too! Yet to see any campaign!MT”@LisaMisol: #Ethiopia journalist #ReeyotAlemu marks 1000th day in prison.
— vineetkhare (@vineetkhare) March 16, 2014
Naamini dunia inamjali pia! Bado nasubiri kuona kampeni yoyote!
#EPRDF government of #Ethiopia continues to show weakness & paranoia as journalist like #ReeyotAlemu scare the daylight out of it. Free her
— MediaET (@MediaETHIOPIA) March 16, 2014
Serikali ya Ethiopia inaendelea kuonyesha udhaifu na hofu wakati waandishi wa aina ya #ReeyotAlemu wanapowasha taa kuimulika. Mwachieni huru
#ReeyotAlemu: why are 3rd world dictators afraid of journos more than death itself? Is a sign of weakness. Scared of ideas & idea people!
— MediaET (@MediaETHIOPIA) March 16, 2014
Kwa nini madikteta wa dunia ya tatu wanawaogopa sana waandishi wa habari kuliko hata kifo? Ni dalili za udhaifu. Wanaogopa maoni mapya na watu wenye maoni.
#Ethiopia – journalist #ReeyotAlemu‘s 1000th day in prison today. She is denied family visits. @SJLambrinidis – why is @EU Ashton silent?
— Ana Gomes, MEP (@AnaGomesMEP) March 16, 2014
Siku ya 1,000 kwa Mwandishi ReeyotAlemu gerezani leo. Amenyimwa haki ya kutembelewa na familia yake. Hivi kwa nini Umoja wa Ulaya iko kimya katika suala hili la Ashton?
March16 marks 1000 days of imprisonment of #ReeyotAlemu & clarifies #ethiopia rule by dictate, injustice & oppression @AnaGomesMEP @amnesty
— EPHREM SHAUL (@eph_sh) March 15, 2014
Machi 16 ni siku ya 1000 ya kifungo cha ReenyotAlemu na inaonyesha namna Ethipia inavyotawala kiimla, uonevu na kwa unyanyasaji
#Ethiopia: #journalism is not terrorism. Free award-winning journalist #ReeyotAlemu, grant her #health care #women pic.twitter.com/UyzmniGrb6
— alex (@alexbiruk) March 16, 2014
Uandishi si ugaidi. Mwachieni huru mwandishi Reeyot Alemu aliyetunukiwa tuzo kibao, mpeni huduma za afya [kama mwanamke]
1 maoni