Mwanamke wa Misri: “Funga Mdomo Wako Obama!”

Video hii ya wanawake wa Kimisri wakimwomba Rais wa Marekani Barak Obama “kufunga mdomo wake” inasambaa sana mtandaoni:

Kwenye video hii, mwanamke ambaye hajatambuliwa anasema kwa Kiarabu kuwa ana ujumbe kwa ajili ya Ombama. Na kisha anabadili lugha na kuanza kuzungumza Kiingereza akisema:

Msikilizeni Obama wenu. Sisi ni wanawake wa Kimisri. Sikiliza Obama. Funga mdomo [akitumia neno la kiingereza ‘mouse’, kifaa cha kuongezea kimshale cha kuelekezea amri za kompyuta] wako. Funga mdomo wako. Sisi sawa. Sisi sawa. Morsi hapana. Morsi hapana.

Sisi ni afisa wa ngazi za juu jeshini Abdel Fattah El Sisi, mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ambaye ndiye anayetangazwa kama Rais ajaye wa Misri wakati Morsi ni mwanachama wa chama cha Muslim Brotherhood ambaye alinyang'anywa urais alioupata kufuatia kuondolewa madarakani kwa Hosni Mubarak mwanzo kabisa mwa Mapinduzi ya Misri.

Na kuna video cha mchanganyiko:

Na kama hiyo haitoshi, kuna picha zinazokufanya ukumbuke nukuu:

Shut Up Your Mouse Obama!

Funga mdomo [Mouse badala ya mouth] Obama!

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.