- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mwanablogu wa Misri Alaa Abdel Fattah Aachiwa kwa Dhamana

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Misri, Habari za Hivi Punde, Harakati za Mtandaoni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza

Mwanablogu anayeheshimika nchini Misri Alaa Abdel-Fattah amechiwa kwa dhamana akisubiri mashitaka leo -baada ya kukaa gerezani kwa siku 115 akidaiwa kuvunja sheria mpya ya kuzuia maandamano.

Kwa muda wote huu, Abdel Fattah amekuwa gerezani [1] bila kesi yake kusikilizwa.

Video hii, iliyowekwa na Mahmoud Salmani inamwonyesha Abdel Fattah akikaribishw ana familia na marafiki zake baada ya kuondoka kwenye kituo cha polisi:

Na Galal Amr anaweka picha hii inayomwonyesha Abdel Fattah akimkumbatia mke wake Manal Hassan:

class=”twitter-tweet” lang=”en”>

Alaa Abdel Fattah (@alaa [2]) ameachiliwa.

Kwenye twiti yake ya kwanza baada ya kuachiwa, Abdel Fattah anajiapiza “kuendelea”[ar]:

“tutaendelea..”

Nadine Marroushi anaitafsiri twiti hiyo:

@_NSalem_ [9] kwa hiyo tafsiri nzuri zaidi; tulipiga rangi hewa kwa kutumia doko. Ni kweli tulifanywa wajinga baadae, lakini tutaendelea.

Doko ni rangi ya kupulizilia kwa lafudhi ya Kimisri.

Zaidi ya Abdel Fattah, Ahmed Abdel Rahman pia aliachiliwa leo. Abdel Rahman, aliyekuwa mpita njia tu wakati wa maandamano, alikamatwa pamoja na Abdel Fattah, alipokuwa akiwasaidia wasichana waliokuwa wanadhalilishwa na polisi.

Kwenye mtandao wa twita, vifijo vilitamalaki.

Ahdaf Souief, shangazi wa Abdel Fattah, anasema kwa furaha:

Mtandao wa twita unalipuka kwa furaha kufuatia kuachiliwa kwa Alaa. Kompyuta yangu ndogo inahitaji mapumziko

Mona Seif, dada wa Abdel Fattah, alifurahia kuachiliwa kwa kaka yake akisema:

Alaa na Ahmed wamerudi mtaani…Hii ni sentensi nzito kuliko zote duniani

Pamoja na hati ya kuachiwa kwake, familia ya Abdel Fattah ilisubirishwa kwa masaa nje ya kituo cha polisi ili kumchukua. Seif anaelezea tabu waliyokumbana nayo:

Tumekuwa tukisubiri nje ya makao makuu ya polisi na hatuelewi sababu ya kuchelewa huku. Baadhi ya waandishi wanatupigia simu kutuambia kuwa vyanzo vyao vya habari vinasema ataachiliwa kesho

Na anaongeza:

Dhamana imelipwa na tumemaliza urasimu wote na Mwendesha Mashitaka wa Serikali na kituo cha pilisi na Ahmed Abdelrahman ameshuka kwenye gari la polisi na amekuwa kwenye kituo cha polisi kwa muda mrefu. Kwa nini kuna ucheleweshaji na kwa nini kuna vikwazo vingi kwa kila hatua?

The case has been adjourned to April 6.