- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Msichana Nchini Madagaska Ajiua Baada ya Picha Zake Kusambazwa Facebook

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Madagaska, Harakati za Mtandaoni, Sheria, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vyombo na Uandishi wa Habari, Wanawake na Jinsia

Koolsaina anaandika kwamba msichana mmoja wa ki-Malagasi alijiua [1] [fr] baada ya picha zake kusambazwa kwenye ukurasa wa Facebook unaoonyesha picha za wasichana wa Madagaska bila ruhusa yao. Wito ulitolewa kwa utawala wa Facebook ulitolewa ili kuufunga ukursa huo. Mpaka leo (Machi 16, 2014), Koolsaina anasema ukurasa huo bado unapatikana.