- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mkutano wa Wanawake wa Nchi Zizungumzao Kifaransa 2014 Wafunguliwa Kinshasa, DRC

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Elimu, Habari Njema, Maendeleo, Mahusiano ya Kimataifa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vita na Migogoro, Wakimbizi, Wanawake na Jinsia
The Banner for the 2014 forum for francophone women in Kinshasa, DRC [1]

Nembo ya mkutano wa wanawake wa nchi zizuingumzao Kifaransa 2014 jijini Kinshasa, DRC – Kwa matumizi ya umma 

Mkutano wa wanawake wa nchi zizuingumzao Kifaransa 2014 [1] [fr] Unafunguliwa leo jijini Kinshasa, DRC. Huu ni mkutano wa pili kufuatia ule uliofanyika Paris mwaka 2013. Wakati ule wa kwanza ulijikita katika kupunguza vitendo vya kudhalilisha wanawake katika maeneo yenye migogoro, lengo la mkutano huu wa 2014 litakuwa ni wajibu wa wanawake katika maendeleo. Warsha tatu zitafanyika [2] [fr]: wanawake na elimu, wanawake na madaraka, wanawake na amani. Majadiliano ya kikundi yatajikita kushughulikia suala la elimu ya wasichana mpaka miaka 16.