Misri Yawahukumu Kifo Wafuasi 529 wa Muslim Brotherhood

A state-of-the-art execution machine designed by @Ternz to help Egypt execute 529 Muslim Brotherhood supporters

Mashine maalumu ya kunyongea iliyobuniwa na @Ternz kuisaidia Misri kuwanyonga wafuasi 529 wa Muslim Brotherhood

Leo, [tarehe 24 Machi] imewahukumu kifo wafuasi 529 wa chama cha Muslim Brotherhood kwa kuhusika na vitendo vya ghasia huko Minya, kaskazini mwa Misri, mwezi Agosti mwaka jana.

Ghasia hizo zililipuka kufuatia kung'olewa madarakani kwa rais wa zamani wa nchi hiyo Mohammed Morsi, ambaye alikuwa kiogozi wa kundi hilo la Muslim Brotherhood leader, na kusababisha mamia ya wafuasi huo kupoteza maisha yao.

Ghasia za Minyah zilisababisha kufa kwa afisa mmoja wa polisi – kosa la jinai ambalo ndilo lililosababisha kushitakiwa kwa washikiwa wote.

Nchini Misri, hukumu hiyo, moja ya hukumu kubwa kabisa ya kifo kuwahi kutolewa katika historia ya leo, ililaaniwa au kuungwa mkono, kutegemeana na mtazamo wa kisiasa wa aliyetoa maoni. Mada Masr alikuwa na orodha ya miitikio hapa.

Mwanablogu wa Misri Zeinobia anasema hukumu hii, ambayo hukumu ya mwisho kabisa inategemewa kusomwa tarehe 28 Aprili, imevunja rekodi mpya ya dunia.

Mwanablogu huyo anaeleza:

Tunayo idadi kubwa ya wagonjwa wa kansa ya damu [Hepatitis C] duniani, tuna idadi kubw aya udhalilishaji wa kijinsia duniani na leo tumevunja rekodi kwa kuwa na hukumu ya kifo kwa watu wengi kwa mpigo kuwahi kutolewa mahakamani katika kesi moja!!! Ninazungumzia kuhusu hukumu ya kihistoria ya mahakama iliyotolewa na mahakama ya jinai ya Minya dhidi ya washitakiwa 529, ndio ile ambayo duniani yote inaizungumzia.

Zeinobia anaongeza:

Nitazungumzia ukweli usiohitaji mjadala hapa :

washitakiwa 529 wamehukumiwa kifo na wengine 15 wakionekana hawana hatia kufuatia kesi ya Minya.
Wengine 139 walishikiliwa kwenye kesi hiyo wakati waliobaki ama waliachiwa kwa dhamana au kwa utaratibu.
Washitakiwa 51 walihudhuria mashitaka hayo mahakamani kwa sababu hapakuwa na sehemu ya kuwawezesha wote kusimama mahakamani kwa wakati mmoja.
Mashitaka hayo yalianza siku ya Jumamosi na kukamilika siku ya Jumatatu.
Wanasheria wa washitakiwa waliomba kubadilishiwa jaji lakini ombi lao lilitupiliwa mbali.
Wanasheria waliokuwa wanawatetea “washitakiwa wasiokuwepo” hawakuruhusiwa kuwatetea washitakiwa !!!
Washitakiwa 529 wametuhumiwa kuwaua msaidizi wa kituo cha polisi cha Matay Sheriff Mostafa El Attar!!
Hii ndio hukumu kubwa zaidi kwa watu wengi kuwahi kutolewa kwa wakati mmoja katika historia ya mahakama za Misri.

Mwandishi wa Misri Bel Trew anashangaa:

Siwezi kufikiri itakavyokuwa wakati wa kuwanyonga watu 529. Kama ilichukua dakika 5 tu kumnyonga mtu mmoja kwa maana hiyo yatahitajika masaa 44 mfululisho kuwanyonga hawa jamaa

Na Mmisri @Ternz, anayekubali kuwa ndio kwanza kaanza kuchora katuni wiki mbili zilizopita, amekuja na suluhisho: Mashine ya kisasa ya kunyongea.

Anaeleza[ar]:

Wakati nikiwa nimepumzisha akili, nikajiuliza: Ninawezaje kulitumikia taifa langu vyema? Ninawezaje kuliletea faida taifa langu na kulisaidia? Kwa hiyo nikachukua kalau na kubuni mashine ambayo Misri inaihitaji wakati huu

Na hapa unaweza kuona ubunifu wake:

Kama mchango wangu kwa taifa langu katika kufanikisha hukumu ya kifo kwa ufanisi, ninatumaini kuwa kifaa hiki kitawavutia maafisa. Hii ni mashine ya kisasa ya kunyongea

Wakati huo huo, mwandishi anayeishi Uingereza, Inigo Gilmore anahitimisha:

Misri inataka watalii warudi, wakati inawabana waandishi mithili ya wanyama; inahukumu mamia ya watu kifo kwa mashitaka bandia?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.