- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mazungumzo ya GV: Namna ya kushinda Ufadhili wa Miradi Midogo ya Rising Voices

Mada za Habari: Amerika Kusini, Ulaya Mashariki na Kati, Guatemala, Hungari, Ugiriki, Harakati za Mtandaoni, Uandishi wa Habari za Kiraia, GV Face, Sauti Chipukizi

Je, unalo wazo la kuisaidia jamii yako kusimulia habari zao kupitia mitandao ya kijamii? Je, unahitaji fedha na msaada? Je, unahitaji kuwa sehemu ya mtandao ya dunia unakusudia kuondoa tofauti ya kidijitali?

Basi unahitaji kutuma maombi kwa ajili ya kupata ufadhili wa miradi midogo ya Rising Voice 2014 [1]!

Ijumaa hii kwenye Mazungumzo ya GV timu ya Mradi wa Global Voices unaosaidia sauti changa kusikika (Rising Voices) itakuwa ikijadili namna bora ya kushinda shindano la ufadhili wa miradi midogo.

Laura Morris, Mhariri wa Rising Voices anaongea na washindi waliopita kutoka Naijer, Guatemala ana Ugiriki kuhusu utaratibu wa kutuma maombi, miradi yao na uzoefu wao wa kuwa sehemu ya jamii ya Rising Voices.G
– Orsolya Jenei, mratibu wa mradi wa Mapping for Niger (Mshindi wa 2013)
– Romeo Rodriguez, mratibu wa mradi wa Xela Civic Libraries Guatemala (Mshindi wa 2012)
– Alexia Kalaitzi, mratibu wa mradi wa Blind Dates, Ugiriki (Mshindi wa 2011)

Kiungo cha tukio hilo kiko hapa.  [2]