- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mazungumzo ya GV: Heri ya Miaka 25 ya Kuzaliwa, Mtandao!

Mada za Habari: Habari Njema, Haki za Binadamu, Harakati za Mtandaoni, Mawazo, Sheria, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Vyombo na Uandishi wa Habari, GV Face

Ni mwaka wa 25 tangu kuzalwia kwa Mtandao wa Intaneti Unaopatikana Duniani kote ujulikanao kama “World Wide Web”! Katika toleo hili la Mazungumzo ya GV, wakongwe wa Global Voices wanazungumzia uzoefu wao wa zamani katika mtandao wa Intenati na yale yote yaliyowezeshwa na mtandao huo katika miaka (karibu) kumi ya shirika hili. Alan Emtage, mtengenezaji wa mtandao na mbunifu wa Archie, mtandao wa kwanza wa kutafutia maudhui kwenye intaneti, anazumngumza nasi kutoka Barbados kuhusiana na uzoefu wake kama mwanzilishi wa Mtandao. Na Kiongozi wa jumuiya wa GV Renata Avila na Mkurugenzi wa Kampeni ya Uandishi Huru wa Mtandaoni Josh Levy wanatuambia kuhusu kampeni ya Mtandao Tunaoutaka,  mradi mpya unaowezesha mazungumzo ya kidunia kuhusu haki za mwanadamu na Mtandao wa Intaneti.