- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kwa nini Maandamano Hayatasababisha ‘Mapinduzi ya Cambodia’

Mada za Habari: Asia Mashariki, Kambodia, Maandamano, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala

Faine Greenwood anaandika kuhusu mhadhara wa Stanford uliotolewa na mwanaharakati wa haki za binadamu wa Cambodia Ou Virak. Aliuliza kuhusu maandamano ya kupinga serikali yanayoendelea nchini Cambodia, Ou Virak alieleza [1] kwa nini hayatasababisha ‘mapinduzi ya kisiasa':

Sidhani kuwa mapinduzi ya Cambondia yatatokea, na wala sidhani yanahitajika…Hatuna hata neno muafaka kwa mapinduzi kwa lugha ya Khmer. Neno la karibu kidogo ni mapinduzi, ambalo huwakumbusha watu neno la lugha ya Khmer “Rouge”.

Alikosoa chama cha upinzani kwa kushindwa kuleta aganda za kisiasa zinazoeleweka:

Sijaona agenda…kitu pekee ninachokiona ni kwa kiasi gani tunamchukia Hun Sen, na namna gani tunaichukia Vietnam…THiyo ni kanuni ya janga, kuendekeza sana chuki. Hatujui tunampigania nani.