- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Korea Kaskazini: Ni Lini Itaanguka?

Mada za Habari: Asia Mashariki, Korea Kaskazini, Korea Kusini, Mahusiano ya Kimataifa, Uandishi wa Habari za Kiraia

Ingawa Korea Kusini inaonekana kutengeneza mahusiano [1] na Korea ya Kaskazini, wataalamu wana wasiwasi kidogo kuhusu kubashiri kuanguka kwa Korea Kaskazini. NKnews.org ilichapisha posti nzuri [2]kuhusu uwezekano wa kutawanyika kwa utawala wa kidikteta, akihitimisha kuwa ‘mageuzi ya kiuchumi ya Pyongyang yanaongeza uwezekano wa tukio la kuanguka vibaya’.