Je, Afrika Kusini ni ‘Nchi Iliyokwama'? Ndivyo Alan Dershorwitz Anavyofikiri

Waafrika Kusini wamekuja juu kuitetea nchi yao baada ya mwanasheria wa Kimarekani na mchambuzi wa duru za kisiasa Alan Dershorwitz kuiita Afrika Kusini kuwa ni “nchi iliyokwama ” wakati akijadili mashitaka ya mauaji ya  Oscar Pistorius  kwenye kipindi cha Piers Morgan kwenye chaneli ya habari ya CNN.

Mwanariadha huyo wa Afrika Kusini asiye na miguu yote miwili  alimpiga risasi na kumwuua rafiki yake wa kike Reeva Steenkamp mnamo Februari 14, 2013; bingwa huyo wa mashindano ya Olimpiki anadai kuwa alidhani anamwuua mtu mhalifu aliyevamia nyumba yake.

American lawyer and political commentator Alan Dershowitz. Photo released under Creative Commons by Flickr user The Huntington.

Mwanasheria wa Marekani na mchambuzi wa mambo ya kisiasa Alan Dershowitz. Picha imetolewa kwa haki miliki ya Creative Commons na mtumiaji wa Flickr aitwaye The Huntington.

Dershorwitz alitoa maoni kwenye mahojiano , “Nimekaa kidogo nchini Afrika Kusini hivi karibuni, na watu hawataki kusikia hili, lakini Afrika Kusini ni nchi iliyokwama.”

Mtazame Dershowitz akitoa matamshi hayo hapa chini:

Muda mfupi baadae, wataalamu wa Uchumi nchini Afrika Kusini walijitokeza kukanusha matamashi hayo, wakisema kuwa nchi ya Afrika Kusini haina vigezo vyovyote vya kuitwa “taifa lililokwama kiuchumi” kama vile ghasia zilizoenea za wenyewe kwa wenyewe, kutokufanya kazi kwa asasi za kiraia, kutokuwepo kwa mhimili wa mahakama unaojitegemea na kutokuwepo kwa ulinzi wa mali za watu.

Waafrika Kusini waliingia kwneye mtandao wa Twita kuonyesha hasira zao na kukana kabisa madai hayo:

Angalieni hali ya mambo nchini mwenu kabla ya kudai Alan #Dershowitz #loser

Afrika Kusini si nchi isiyona dosari, wala haikaribii. Lakini hata hivyo, nani hana dosari? Lakini #Dershowitz alizungumza kwa upande wa kijinga na akijifanya bora. Hilo ndilo suala

#Dershowitz anahitaji kupunguza kuangalia televisheni. Ana ile hulka ya kuiona Afrika kama nchi. Kweli elimu ya sheria haitibu maradhi ya ujinga

#Dershowitz ameonyesha mkanganyiko wa wa kurithi kimantiki Marekani; kuifanya Afrika kuwa ya kizamani na kuiona Afrika Kusini kuwa yenye uchafu wa kimaadili

Mheshimiwa Alan #Dershowitz Afrika Kusini iko mbali sana kuwa nchi iliyokwama. Nchi inayoendelea labda, lakini haijakwama

Hoja za #Dershowitz unafanya muhtasari tu wa mtazamo au imani kwamba Afrika bado mengi ya kuogopa kutoka kwa “marafiki” zake

Some Twitter users took the opportunity to show Deshorwitz that the US is not a perfect state:

#Dershowitz anasema nyie nyote mnaoishi isiyo na udhibiti wa bunduki na mahali ambapo watoto hawako salama kwenda shule, inaweza kuwa ya kijinga tu!!!

#Dershowitz, ni bora niishi kwenye nchi yangu [Afrika Kusini] yenye kila namna ya tofauti na changamoto kuliko hulka yenu Wamarekani kujiona bora

Wamerikani wanaifanya dunia isiwapende, na wana rais poa! Raia wake mmoja aliyeoza anaharibu nchi

#Dershowitz anatuita watu tusiheshimu sheria na tulikwama? Marekani inalipua nchi nyingi na inataka kumtawala kila mtu. Kweli sema unachotaka, wala hiyo haimaanishi kuwa Marekani ina maadini ya kutufundisha wengine

Hivi inakuwaje kuishi kwenye nchi ambapo bunduki zimetawanyika, nchi ya kibepari na inayojifanya “inamwogopa mungu” Bw #Dershowitz?

#Dershowitz unathubutu vipi kutingisha kichwa chako na shingo yako nyekundi na kututukana wazi wazi sisi wote kama taifa! Vipi Marekani na ubaguzi wake wa rangi na uhalifu?

Mtumiaji mmoja akatania:

Nadhani tunahitaji Marekani iivamie Afrika Kusini ili kurekebisha hali hii ya nchi kushindwa, ha ha. Ah, subiri kidogo, kumbe hatuna mafuta, ah! *Gida mvinyo kidogo*

Hata hivyo, wachache waliafikiana na Dershowitz:

Ha! kwa hiyo kama ningeingia kwenye mtandao wa twita nikiunga mkono mahojiano ya #Dershowitz basi ningechukiwa sana sio? Lakini kwa kiwnago fulani JAMAA YUKO SAHIHI!

#Dershowitz nitakubaliana kabisa na wewe KUWA AFRIKA KUSINI NI NCHI ILIYOKWAMA NA ISIYOONGWA KWA SHERIA, wahalifu wanatembea kifua mbele na hata Oscar hatakwenda jela ingawa tunajua ni muuaji

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.