- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Iran: Mwanafunzi Ahukumiwa Miaka 7 Jela

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Iran, Maandamano, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Utawala

Blogu ya PersianBanoo iliripoti [1] kuwa “mwanafunzi mwanaharakati wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Qazvin aliyefukuzwa, Maryam Shafipour amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela. Awali iliripotiwa na familia yake kuwa alikuwa amepigwa na maofisa wa kiume waliokuwa wanamhoji wakati wa kuhojiwa kukiendelea”.