- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Fasiri ya Lugha ya Kikannada ya Karne ya 11 Yapatikana kwenye Mfumo wa Wikisource

Mada za Habari: Asia ya Kusini, India, Fasihi, Historia, Sanaa na Utamaduni, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia

Vachana Sahitya [1] ni aina ya uandishi kwa mtindo wa sauti katika lugha ya ki-Kannada [2] ambao ulianzia karne ya 11 na kukua sana kwenye karne ya 12. Makala ya Subhashish Panigrahi [3] inaripoti (ikiwa imeandikwa kwa ushirikiano wa Pavithra Hanchagaiah na Omshivaprakash) kwenye blogu ya Wikimedia kwamba waandishi wawili wa Wikimedia wakishirikiana na mtaalamu wa lugha ya ki-Kannada wamegeuza beti 21000 za Vachana Sahitya katika mfumo wa Unicode na hiyo kwa sasa zinapatikana [4] kwneye Wikisource, maktaba ya kidigitali ya mtandaoni ambayo ina maudhui ya nyenzo za maandishi yanayopatikana bure.