Serikali ya Uturuki imeufunga mtandao wa Twita -sambamba na huduma ya Google iitwayo DNS [1], iliyokuwa inatumika kama njia ya mzunguko kufuatia kufungwa kwa mtandao wa twita. Inaonekana, hata hivyo, kuwa mpango wa serikali hiyo wa kudhibiti raia wa nchi hiyo kuwasiliana unakumbana na mipango kinzani, kwa kuwa twiti zinazotoka nchini Uturuki ndio kwanza zimeongezeka.
Kufungiwa kwa mtandao wa Twita, kulikoripotiwa kuathiri watu zaidi ya milioni 10 wanaotumia mtandao huo nchini Uturuki, hali iliyofuatia kuchapishwa kwa nyaraka zinazosemekana ‘kufunua’ ufisadi wa maswahiba wa karibu wa Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan.
Taarifa za habari zinasema [2] kuwa Erdogan ameahidi “kuufutilia mbali mtandao wa Twita” akiongeza kuwa kamwe hajali kile ambacho kingesemwa na jumuiya ya kimataifa.
Juan Cole anaelezea [3] jaribio la Erdogan la kufungia huduma hiyo ya kijamii akiita “upuuzi”:
Jaribio la kipuuzi la Erdogan la kujaribu kudhibiti matumizi ya mtandao wa intaneti limekwama na kushindwa mara moja. Vijana wa Kituruki wana weledi kuhusiana na matumizi ya zana za kupata huduma hiyo ziitwazo Tor na VPN, na watumiaji wa Twita nchini Uturuki walijipanga haraka sana kiasi ambacho huenda kilimchanganya kichwa ndugu Erdogan.
Erik Meyersson anaongeza:
#Turkey [4] tweeps discovered @torproject [5] last year, no surprise ppl still tweeting despite #TwitterisblockedinTurkey [6] pic.twitter.com/Exz3kVh91l [7]
— Erik Meyersson (@emeyersson) March 23, 2014 [8]
Watumiaji wa mtandao wa Twita nchini Uturuki walimgundua @torproject [5] mwaka jana, haishangazi watu bado wanatwiti pamoja na kufungiwa kwa mtandao huo nchini Uturuki
Na mtafiti wa Uturuki Zeynep Tufekci anatabasamu muda wote amvao watumiaji wa mtandao wa twita nchini Uturuki wanapaza sauti zao pamoja na kufungiwa kwa mtandao huo:
:-) “despite”=”because of” RT @mashable [9] Whoa: 1.2 million tweets sent in Turkey, despite ban http://t.co/P7MIhx6Vhr [10] pic.twitter.com/OKzxHFcALT [11]
— Zeynep Tufekci (@zeynep) March 21, 2014 [12]
Ingawa mtandao umefungiwa bado twiti milioni 1.2 zimeendelea kutumwa nchini Uturuki
Hata hivyo, anaongeza:
A DNS block, followed by a patchy IPS block, then who-knows-what. Turkey is on its way to high tech literacy. Next up, grandmas on Tor.
— Zeynep Tufekci (@zeynep) March 23, 2014 [13]
Kufungiwa kwa DNS, ikifuatiwa na kufungiwa kwa IPS, nani ajuaye nini kinafuata. Uturuki iko mbioni kuwa na weledi wa hali ya juu wa masuala ya kiteknoloji. Kinachofuta ni mradi wa Tor
Kutoka Uturuki, Engin Onder anaeleza namna watumiaji wa Twita walivyosambaza ujumbe wa namna ya “kuuzunguka” ufungiaji huo:
#twitter [14] blocked in #turkey [15] tonight. folks are painting #google [16] dns numbers onto the posters of the governing party. pic.twitter.com/9vQ7NTgotO [17]
— Engin Onder (@enginonder) March 21, 2014 [18]
Mtandao wa twita umefungiwa leo nchini Uturuki, jamaa wanatengeneza huduma ya DSN ya google kwenye mabango ya chama tawala