Changamoto za Fedha katika Kufadhili Tafiti za Kisayansi Ufaransa, Nchi za Kiafrika

Ni nadra sana kuupuuza umuhimu na nafasi ya tafiti za sayansi katika kuleta maendeleo ya nchi. Hata hivyo, ikitokea umuhimu huo kuupuzwa, mara nyingi athari huwa si za moja kwa moja, au huwa za moja kwa moja lakini zenye madhara ya muda mrefu. Kwa hiyo tatizo la manufaa yanayotokana na tafiti na ugunduzi unaofanyika kama matokeo ya tafiti hizo kuwa ya kati ya muda mfupi hadi wa kati, bado yapo kwa nchi nyingi.

Upatikanaji wa fedha kwa ajili ya tafiti hufuata kanuni kadhaa hususani kwa fedha zinazotoka kwenye sekta ya umma au ya binafsi. Nchini Ufaransa, ili tafiti zozote za umma zifanikiwa, Shirika la Taifa la Utafiti nchini humo [French National Research Agency] linaeleza namna utafiti unavyoweza kufadhiliwa nchini humo [fr]:

Les laboratoires de recherche publics sont en partie financés par les crédits budgétaires des universités, des organismes de recherche publics et des agences de financement, dont l'Agence nationale de la recherche (A.N.R.). Ils bénéficient d'autres dotations provenant des régions françaises, des associations caritatives, de l'industrie et de l'Europe. […] 7 000 projets financés rassemblant plus de 22 000 équipes de recherche publiques et privées entre 2005-2009 et le montant cumulé des financements 2005-2009 est de 3 milliards d'euros.

Maabara zinazotumika kwa tafiti za umma bado hazipati fedha za kutosha kutokana na mafungu ya bajeti yanayotengwa na vyuo vikuu, vyombo vya utafiti vya umma, na mashirika ya fedha, kama vile Shirika la Taifa la Utafiti nchini Ufaransa. [Maabara hizo] hunufaika na fedha zinazotengwa na majimbo ya kiutawala nchini Ufaransa, mashirika ya misaada ya hisani, viwanda na hata kutoka [Tume ya Umoja wa] Ulaya […] miradi 7,000 ilifadhiliwa, ikiziwezesha timu za watafiti wa umma na binafsi zipatazo 22,000 kati ya mwaka 2005-2009. Jumla ya fedha zilizotolewa katika kipindi hicho ni Euro Bilioni tatu.

Public research funding in France - Public domain

Mchoro unaoonyesha namna fedha za utafiti zinavyopatikana nchini Ufaransa – Kwa matumizi ya umma.
Tafiti nchini Ufaransa zinafadhiliwa na vyuo vikuu, vyombo vya tafiti, na Shirika la Utafiti la Taifa(ANR). Lakini pia hupata michango kutoka kwenye viwanda vya madawa na Tume ya Ulaya.

Pamoja na juhudi zinazotokana na serikali za kuhamasisha upya sekta hiyo [fr], tafiti zinazofanyika nchini Ufaransa zina hali mbaya ukilinganisha na zile za majirani zao wa nchi za Ujerumani na Uingereza na kwa hakika zinaonyesha dalili za kuzorota na uwezekano wa kupotea kabisa. David Larousserie anaonyesha bashiri yake kuwa [huenda] tafiti za sayansi nchini Ufaransa zina ushindani lakini hazileti tija vya kutosha, katika makala yake yenye kichwa cha habari “Uwezeshaji usioridhisha wa fedha kwa ajili ya tafiti za umma” [fr]:

Les experts soulignent aussi “les bonnes performances en recherche de la France” mais les jugent “moyennes en termes d'innovation et de retombées économiques”. La France publie beaucoup (6e rang mondial) et dépose bon nombre de brevets (4e rang sur les dépôts en Europe), mais des indicateurs “d'innovation” la placent au 24e rang.

Wataalam vile vile wanasisitiza “ufanisi mzuri wa tafiti nchini Ufaransa” lakini wanauona kuwa “wa wastani kwa maana ya ubunifu na faida ya kiuchumi”. Ufaransa huchapisha nyaraka nyingi za kutangaza ugunduzi unaofanywa na watafiti (ni ya sita duniani) na huweka kumbukumbu nzuri ya taarifa hizi (ya nne barani Ulaya) lakini ya 24 kwa mujibu wa viashiria vya “ugunduzi”.

Anaongeza kwamba:

Pour expliquer la réduction des marges de manœuvre en dépit d'une enveloppe globale en croissance, les magistrats rappellent que la cause essentielle est l'augmentation des frais de personnel dans les organismes de recherche. Au CNRS, avec des effectifs de fonctionnaires stables, la subvention publique a augmenté de 293 millions d'euros entre 2006 et 2011

Katika kuelezea kuondoshwa kwa uwezekano wa udanganyifu pamoja na kuongezeka kwa bajeti ya kidunia, inaonyesha kuwa sababu ya msingi ni kuongezeka kwa gharama za wataalam katika mashirika ya utafiti. Katika Shirika la Utafiti la Taifa nchini Ufaransa (CNRS) kwa mfano, pamoja na kuwa na nguvu kazi imara, ruzuku kutoka serikalini iliongezeka kwa euro 293 bilioni kati ya mwaka 2006 na 2011.

Wengine wanafikiri kwamba kuna sababu nyingine zinazohusika, kama Fauconnier, anayeamini kuwa uratibu baina ya mashirika tofauti ya utafiti unaacha maswali mengi bila majibu [fr]:

Quand on veut monter une Unité mixte de recherche (UMR), la structure qui permet de partager des contrats de recherche, par exemple entre une université et le CNRS, beaucoup de temps et d’argent sont gâchés en gestion de problèmes administratifs complexes.

Tunapotaka kujenga kitengo cha pamoja cha utafiti (UMR), mfumo unaosaidia kushirikishana mikubaliano ya kiutafiti (kati ya chuo kikuu na shirika la utafiti la Ufaransa (CNRS) kwa mfano, muda mwingi na fedha vinapotea katika kushughulikia matatizo mengi yanayotokana na mambo ya kiutawala.

NASA researchers on Project Stardust - Public domain

Watafiti wa NASA kwenye Mradi wa Stardust – Kwa matumizi ya umma

Utafiti barani Afrika

Kama kwa nchi kama Ufaransa utafiti unakumbana na matatizo ya kifedha, hali inatarajiwa kuwa tete katika nchi nyingi za ki-Afrika. Hata hivyo Afrika Kusini inaonekana kuwa kwenye nchi bora 30 katika uwekezaji unaofanywa kwenye tafiti na maendeleo(R&D). Inasikitisha kuwa, hakuna nchi yenye kuzungumza Kifaransa inayoonekana kwenye orodha ya nchi 70 zinazowekeza kwenye tafiti za kisayansi.

Juian Siddle, kwa upande wake anaeleza kwamba bara la Afrika lina kila kinachohitajika kuweza kuwa kituo kikuu cha sayansi duniani:

Msingi unaohitajika upo -yaani ufahamu, utayari wa kujifunza na kuendana na mazingira halisi, ikiwa ni pamoja na upanukaji wa kasi wa teknoloji ya dijitali. Vyote hivi vinaiwezesha Afrika kutimiza wajibu wake kikamilifu katika kushirikiana na sehemu nyingine duniani.

Calestous Juma, profesa wa Maendeleo ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Harvard, anaongeza kwamba mazingira ya bara la Afrika yako tofauti:

Mweleko wa kimkakati kwa Afrika wapaswa kuwa katika kuwezesha kufanyika kwa tafiti ambazo zinafaida ya kutatua matatizo yanayozikabili jamii hizo kwa wakati husika. Ni kwa kupitia mikakati hiyo kwamba Afrika inaweza kuchangia kipekee katika tasnia ya sayansi duniani

Chemistry lesson in Kenya from un.org, with their permission

Kipindi cha somo la Kemia kutoka kwenye tovuti ya un.org, imetumika kwa ruhusa

Je, tunasaidia utafiti kweli?

Lakini labda, pamoja na uwezekano wa kupatikana kwa msaada kutoka katika serikali nyingi, tafiti za kisayansi zinakosa uungwaji mkono na watu, hali ambayo ingeweza kusaidia kushinikiza wanasiasa kuwezesha tafiti kifedha kwa namna endelevu zaidi. Hiyo ni hoja ya John Skylar, katika makala inayojibu madai ya ukurasa unaosambaa mtandaoni unaoitwa “Naipenda sana Sayansi”, lakini kiukweli nchi chache ziko tayari kuwekeza katika tafiti zinazokidhi viwango: 

Mwenendo wa mambo kwa zaidi ya miaka 10 hadi 20 iliyopita, unaonyesha kudorora kwa kasi kwa mafungu ya fedha za kuendeleza sayansi kutoka serikalini. […] Unajua kuwa bajeti halisi za nchi zetu haziendani na hali hii? Kwa mfano kama ungekuwa na mapenzi na sekta ya sayansi, kura yako ungempa mgombea wa nafasi ya kisiasa mwenye utashi wa kufadhili sayansi. Ungeifanya sayansi kuwa suala linaloibua mijadala mikali katika vyombo vya habari, kwa kiwango kiwango kile kile kinacholingana na mijadala ya vita na misuguano ya kisiasa

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.