Aliyoyaandika Waziri Mkuu wa Urusi Medvedev Kwenye Mtandao wa Facebook Kuhusu Ukraine

"Dmitry Anatolyevich, are you sleeping again? Dmitry Anatolyevich?" Anonymous image found online.

“Dmitry Anatolyevich, umelala kwa mara nyingine?Dmitry Anatolyevich?” Picha isiyojulikana imewekwa na nani mtandaoni.

Waziri Mkuu Medvedev, ambaye amekuwa kimya kuhusu hali ya mambo nchini Ukraine kama mkuu wake wa kazi Rais Putin, hatimaye alichagua mahali pasipotarajiwa kusemea alipofikia uamuzi wa kutoa tamko. Yeye mwenyewe, au moja wapo wa makatibu wahutasi wake, waliandika [ru]  kwenye ukurasa wake wa Facebook, andiko ambalo tayari limepata miitikio zaidi ya 5,000 na kuvutia zaidi ya watu 6,000 pamoja na kutawanywa zaidi ya mara 3,000. Katika andiko hilo alitoa matamko kadhaa, lisilotarajiwa kabisa likiwa hili:

Да, авторитет президента Януковича практически ничтожен, но это не отменяет того факта, что по Конституции Украины он – легитимный глава государства.

Ndio, mamlaka aliyonayo Rais Yanukovich kihalisia hayapo, lakini hiyo haibadili ukweli kwamba, kwa mujibu wa katiba ya Ukraine, bado ni mkuu halali wa nchi hiyo.

Aliendelea kupendekeza kuwa Bunge la Ukraine inabidi lipige kura ya kutokuwa na imani na Yanukovich, kama hicho ndicho wanachotaka kukifanya. Maelezo haya kuhusu mamlaka ya Yanukovich yaliwafanya baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Twita kutoa maoni kuhusu msimamo huo wa Medvedev.

Arnold Schwarzenegger and Dmitry Medvedev with swapped heads. Anonymous image found online.

Arnold Schwarzenegger akiwa na Dmitriy Medvedev wakiwa wamebadilishwa vichwa. “Mapacha” kwa kinyume. Picha hii haijulikani imewekwa na nani mtandaoni.

Twiti moja ambayo imetumwa kwa mara nyingine kwa zaidi ya mara 150 ilitania:

Wakati vita vinaendelea, Medvedev anaishi kwa bibi (nyanya) yake

Mwanablogu mwingine alitwiti:

Medvedev amempata mtu ambaye ana lawama zaidi kuliko alivyo yeye, na anaendelea kujaribu kuruka ruka kwenye maiti za kisiasa  

Wengine waliona kuwa rais halali mwenye mamlaka sifuri ni sawa na “upuuzi [ru].”

"Don't worry Vic[tor], we've got this." Anonymous image found online.

“Usiogope Victor, tumepata hiki.” Picha isiyojulikana imewekwa na nani mtandaoni.

Wakati huo huo, Medvedev alimaliza bandiko lake kwenye mtandao wa twita kwa kuiita Ukraine “jirani masikini”: 

России нужна сильная и стабильная Украина. Предсказуемый и экономически состоятельный партнер. А не бедный родственник, вечно стоящий с протянутой рукой.

Urusi inaihitaji Ukraine iliyo imara na yenye utengemavu wa kisiasa. Ukraine iliyo rafiki anayetabirika na mwenye uchumi imara. Sio ikiwa jirani masikini, siku zote ikisubiri mkono wa kuinusu.

Miitikio ya bandiko hilo yanaanza na maneno chanya kama (“Ndiyo, ninakubali” na “Umesema sawasawa”), lakini haraka yanageuka kukosoa msimamo wa Urusi kwa hali ya Ukraine na hatua yake ya kuivamia kijeshi Crimea. Medvedev, au timu yake ya mawasiliano, haijajibu chochote kwa lolote lililoandikwa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.