- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wiki ya Mitandao ya Kiraia Jijini Lagos 2014

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Naijeria, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia

Wiki ya Mitandao ya Kiraia jijini Lagos 2014 [1] (Februari 17-21) inaendelea jijini Lagos, Niajeria:

Wiki ya Mitandao ya Kiraia Lagos ndio kwanza mwaka wake pili kufanyika na tayari imepata umaarufu kama mkutano mkubwa zaidi wa kiteknolojia, mitandao ya kijamii na kibiashara barani Afrika. Tukio hilo limevutia wanazuoni maarufu, bidhaa maarufu, watu wajifunzao na wabunifu maarufu. Likiwa na idadi ya watu wapatao milioni 20, Lagos ndilo jiji kubwa la watu weusi duniani na inasemekana ni kitovu cha bara la Afrika na makazi ya makampuni makubwa ya kibiashara na kiteknolojia katika bara la Afrika. Kw akutambua umuhimu wa bara hili kuunganishwa, na kuhamasisha ushirikiano, dhima kuu ya mkutano wetu wa mwaka 2014 ni: AFRIKA ILIYOUNGANISHWA NDIYO MUSTAKABALI.

Tukio la pekee na la aina yake, Wiki ya Mitandao ya Kiraia Lagos ni mkutano wa kidunia unaohudhuriwa na watu wenye bongo zinazochemka kwa kiwango cha kidunia ambao hauna kiingilio na uko wazi kwa yeyote. WMK Lagos ni wa pekee kwa sababu asilimia 70 ya majopo, dhifa na warsha zimeandaliwa na umma