Warusi “Wapuuza” Olimpiki na Kufuatilia Ghasia za Ukraine

A woman in Kiev reacts to the sight of two dead bodies (protesters killed in the violence). 18 February 2014. Screenshot from YouTube.

Mwanamke mjini Kiev akishtuka baada ya kuona miili ya maiti wawili (waandamanaji waliouawa katika ghasia) za Februari 18, 2014. Picha imepigwa kwenye mtandao wa YouTube.

Kabla ya kuanza kwa Mashindano ya Sochi ya Majira ya Baridi takribani majuma mawili yaliyopita, mwandishi aliyejitambulisha kama wako mkweli (yours truly) aliliambia shirika la Habari za Kimataifa la Marekani kwamba gahsia zinazoendelea nchini Ukraini zingeweza kubadili uelekeo wa ufuatiliaji wa mashindano ya Olimpiki kwa Warusi wanaotumia Intaneti. Leo, baada ya ghasia na vurugu kuanza tena kwenye mitaa ya Kiev, na kugeuza kabisa upepo wa habari katika mitandao ya kiRusi. Kwa hakika, picha zinazokuja kutoka Ukraini zinachora taswira ya kitu kinachofanana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Wakati habari kutoka Kiev zikigonga vichwa vya habari duniani kote, uchambuzi wa matumizi ya mtandao wa Twita yanaonyesha kwamba matukio yanayoendelea leo nchini Ukraine yamekamata hisia za wazungumzaji wa Kirusi kuliko sehemu nyingine yoyote duniani. Kwa hakika, katika masaa 24 yaliyopita kwenye mtandao wa Twita, hamasa ya watumiaji wa Twita wa Ki-Rusi katika kufuatialia hali ya mambo nchini Ukraini imezidi bashasha ya kufuatilia mashindano ya Olimpiki. Hali hii inabadili mwelekeo uliokuwepo tangu Januari 25, 2014, majuma kadhaa kabla ya kufunguliwa rasmi kwa mashindano hayo, ambapo wa-Rusi wali-twiti zaidi kuhusu Kiev kuliko Sochi, mahali yanakofanyikia mashindano ya Olimpiki.

Takwimu za watumiaji wa Twita baina ya wazungumzaji wa Kiingereza kwa zaidi ya mwezi uliopita zinaonyesha hali hiyo hiyo, lakini hamasa ya kujua kinachoendelea Sochi imekuwa juu siku zote. Hata leo, Ukraine ikiwa inawaka moto, twiti za Kiingereza kuhusu Kiev zimezidi kidogo nusu ya zaidi ya twiti laki mbili kuhusu Mashindano ya Olimpiki.

Wakati haishangazi kwamba watumiaji wa Intaneti wamevutwa na harakati za kimpinduzi huko Kiev, inashangaza kwamba wenyeji wa mashindano ya Olimpiki wamepoteza hadhira yao kwa tukio la nje ya nchi hiyo.

Twiti za ki-Rusi(bofya kukuza):

Russian-language tweets about “maidan” or “kiev” (orange) versus tweets about “sochi” or the “olympics” (blue).

Russian-language tweets about “maidan” or “kiev” (orange) versus tweets about “sochi” or the “olympics” (blue).

Twiti za ki-Rusi kuhusu ghasia za “kiev” (rangi ya chungwa) na twiti za “sochi” ama “Olimpiki” (bluu).

Twiti za Kiingereza (bofya kukuza):

English-language tweets about “maidan” or “kiev” or “euromaidan” or "kyiv" (orange) versus tweets about “sochi” or the “olympics” (blue).

English-language tweets about “maidan” or “kiev” or “euromaidan” or “kyiv” (orange) versus tweets about “sochi” or the “olympics” (blue).

Twiti za Kiingereza kuhusu ghasia za “kiev” (rangi ya chungwa) na twiti za “sochi” ama “Olimpiki” (bluu).

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.