Venezuela Nitakayoikumbuka Daima

Caracas

Caracas, Venezuela. Picha kwa hisani ya mtumiaji wa flickr danielito311. Used with Creative Commons licence (BY-NC 2.0).

Nikikumbuka Peru, ukatili na hofu vilikuwa ni sehemu ya maisha yetu

ndio nilikuwa nimemaliza elimu yangu ya sheria jijini Lima. ilikuwa ni mwaka 1993 na ambapo wakati huo Peru yangu niipendayo ndiyo ilikuwa inajijenga mara baada ya miaka 12 ya machafuko ya wenyewe kwa wenyewe  yaliyogharimu maisha ya makumi elfu ya watu.

Krismasi ilikuwa inakaribia na kwa mara ya kwanza niliamua kumtembelea shangazi yangu kipenzi. 

Dada mkubwa wa mama yangu alihamia Venezuela miaka ya 1950. aliolewa huko Caracas na aliishi huko na mumewe pamoja na watot wao wawili wa kiume. mara baada ya binamu wangu mdogo kufariki katika ajali ya gari, mama yangu na dada yake waliimarisha ukaribu wao, na kamwe hawakuruhusu umbali uwatenganishe.

Nilipofika Simón Bolívar International Airport [es] Maiquetía, haraka nilishangazwa na namna ambavyo mambo yalivyokuwa tofauti, haswa nilipolinganisha na Lima.

Caracas ulikuwa ni mji uliokuwa unapendeza, wenye majengo marefu, barabara kuu, barabara za kupandana, na barabara zilizokuwa zimefanyiwa ukarabati siku za karibuni.

magari yote yalionekana kana kwamba ndio yametolewa kiwandani, yenye kung'aa na ya kifahari; Magari mapya ni jambo tililokuwa tumeanza kulizoea Peru, baada ya mfumuko wa bei usiozuilika [es] uliotuacha wengi wetu kama mabilionea tusiokuwa na uwezo wa kununua chochote.

alama z barabarani zilionekana kana kwamba ndio ziliandikwa jana tu.

niliweza kuhisi maendeleo kila nilipopatazama, na hiii ilikuwa ni katika safari yangu ya kutoka uwanja wa ndege kulekea nyumbani kwa shangazi yangu. Katika safari hii, mvua ilinikaribisha, kitu ambacho sisi watu wa Lima hatukukizoea kabisa.

siku iliyofuata nilianza kulitembelea jiji. sikujiona kama mgeni kabisa. Jamii yangu ilikua ikiangaliaMy generation grew up watching Venezuelan soap operas on TV, kwa hiyo baadhi ya maeneo maarufu yalikuwa siyo mageni kwangu: Chacao, Chacaíto, Bikira wa Chiquingirá. kwa hiyo, yalikuwa ni maongezi ya mahadhi niliyoyagundua yaliyokuwa yakinifuata kila nilipokuwepo,  baada ya siku chache.

katika kutembelea nyumba fulani ya maonesho, nilimuona jamaa mmoja akitazama orodha ya mapambano yaliyopiganwa na Simón Bolívar, ambaye ni mpigania uhuru wa Venezuela, Colombia, Ecuador, Perú and Bolivia. kulikuwa na majina ya mapambano pasipo kuwa na kiashiria cha mahali ambapo mapambano hayo yalipofanyikia, na nilisimama pembeni mwa mtalii huyu na kisha nilianza na somo nililojifunza shuleni miaka mingi iliyopita: Carabobo, Venezuela; Boyacá, Bogotá, Pichincha, Ecuador; na Junín na Ayacucho, Perú (nchi yako kwa hakika).

katika safari hiyo, wakati wa matembezi katika pwani ya bahari ambayo jina lake nimelisahau, vidole vyangu vilihisi maji ya bahari ya Atlantic, hali inayonikumbusha pia Venezuela.

Lakini kilichonifurahisha zaidi kilikuwa ni uhuru waliokuw nao watu, walikuwa wakiishi maisha waliyoyataka. tuliweza kuingia katika jengo lolote na bila ya kukutana na askari yeyote aliyekuwa akisubiri kutukagua na mali zetu. Hakukuwa na vifaa vya kutafuatia vitu vya chuma alivyobeba mtu wala uwepo wa mashine maalum ambazo tulipaswa kupita kwanza katika milango ya maduka, katika majumba ya maonesho na mambo mengine yanayohusiana na hayo.

Pia nilipita katika majengo ya serikali na ya wizara mbalimbali, kana kwamba hilo lilikuwa ni jambo la kawaida kabisa. hakuna aliyenikataza kuwepo maeneo yale, hakuna aliyetaka kuangalia taarifa zangu, na hakuna yeyote aliyetaka kunifanya nihisi kuwa kulikuw na jambo la kuogopa.

Hii ndio sababu inayonifanya nigubikwe na huzuni, kufuatia habari za hivi karibuni pamoja na picha zinazotumwa kutoka Venezuela

Watu wa Venezuela wanahangaika. Watu wa Venezuela  wanalia. Watu wa Venezuela  wanaomboleza.

Waandamanaji wanapigania uhuru wa kuishi watakavyo na kushinikiza haki ya kuheshimiwa. Vijana wadogo wanakufa mitaani kufuatia mapambano kati ya waandamanaji dhidi ya polisi na wafuasi wengine wa serikali. Ndugu wanapigana dhidi ya ndugu wenzao. 

Ninapendelea kuikumbuka Venezuela ya mwaka 1993 niliyoifahamu. Mirindimo ya muziki wa Caribbean wenye kufurahisha pamoja na nyimbo za kitamaduni za Krismasi popote nilipokwenda. Nyiso za furaha zilizokuwa zikiniamkia, watu walinikaribisha kwa moyo mmoja, hadi nilipokuja kujifunza kuwa nilikuwa mtu wa Peru. 

Venezuela, utaendelea kuwa ndani ya moyo wangu.

Gabriela Garcia Calderon ni mwanasheria mwenye asili ya Peru aliyebobea katika masuala ya Usuluhishi na Haki za Raia. Amekulia kwenye familia yenye asili ya kujihusisha na masuala ya habari huko Peru. Gabriela amekuwa mwandishi wa Sauti za Dunia (Global Voices) tangu Novemba 2007.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.