- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Upasuaji wa Kwanza wa Moyo Kongo Brazzaville

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Jamhuri ya Kongo, Ufaransa, Afya, Habari Njema, Habari za Hivi Punde, Maendeleo, Mahusiano ya Kimataifa, Mwitikio wa Kihisani, Safari, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vijana
Child awaiting heart surgery via La chaine de l'espoir with their permission [1]

Mtoto akingojea upasuaji wa moyo. Picha kwa hisani ya La chaine de l'espoir imetumiwa kwa ruhusa yao

Mtandao wa kimataifa wa Afya La Chaîne de l’Espoir (Maana yake Kiungo cha Matumaini) unaripoti kuwa watoto saba wa ki-Kongo waliokuwa na hali mbaya wamenufaika na upasuaji wa moyo [fr] [2] uliofanyika Februari 14 mjini Brazzaville, Kongo. Kwa msaada wa Msaidizi wa Kongo Shirika lenyewe, Prince Béni na Maya, wote wakisumbuliwa na maradhi ya moyo walifanyiwa upasuaji kwa masaa kadhaa kama ripoti ifuatayo inavyosema [3] [fr]:

Elle a dix ans et ne pèse que quinze kilos. Son cœur fonctionne mal. Il l'empêche de s'alimenter et donc de grandir. La petite fille doit être opérée le plus vite possible. L'intervention dure six heures.

(Mayala) ana umri wa miaka kumi na ana paundi 15. Moyo wake haufanyi kazi ipasavyo. Unamzuia kupeleka virutubisho kwenye seli zake na hivyo kuleta matatizo ya ukuaji hafifu. Msichana huyu alihitaji upasuaji wa haraka. Na upasuaji huo ulifanyika kwa masaa sita.