- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Theluji Nchini Iran: Watu 500,000 Wakosa Umeme, Nishati ya Gesi Pamoja na Maji

Mada za Habari: Uandishi wa Habari za Kiraia
Snow in Mazandaran. Source: Mehr. Photographer: Pejman Marzi.

Theluji huko Mazandaran. Chanzo: Mehr News Agency. Mpiga picha: Pejman Marzi.

Inataarifiwa kuwa watu 500,000 wameshindwa kutoka katika vijiji wanavyoishi huku wakikosa huduma ya umeme, nishati ya gesi pamoja na maji [1] hali iliyotokana na kutanda kwa theluji mwisho wa wiki hii Kaskazini mwa nchi ya Iran katika majimbo ya, Gilan [2] na Mazandaran [3].

Afisa mmoja alisema kuwa hili ni anguko kubwa la theluji ambalo halikuwahi kutokea kwa miaka 50 iliyopita [4]. Hadi sasa, maelfu ya watu wameshaokolewa na kupelekwa kwenye makazi ya muda au kulazwa hospitalini.

ZA1-1RA alitwiti [5]:

Sina shaka na familia yangu, wana hifadhi ya kutosha ya mchele kwa matumizi ya miezi kadhaa.

Farshad Faryabi alitwiti [9]:

Waziri wa mambo ya nje wa Swiden, Carl Blidt, [aliyeko safarini nchini Iran] hataweza kurudi Swiden kutoka na hali tete ya theluji nchini Iran.

Soheila Sadegh alitwiti [14]:

Theluji nzito yaharibu vibaya shule huko Gilan.

Maysam Bizar alitwiti [25]:

Gharama ya maji ya chupa yalipanda mara nne zaidi ya bei ya kawaida katika kipindi cha tatizo la theluji. Kama hatuwezi kujihurumia, labda cha kufanya ni kutegemea maadui?

Mozdeh A alitwiti [28]:

Kilicho na Baraka kwa wengine, kwetu ni laana.

Saham Borghani mwezi uliopita (tar 10 Januari) aliweka [30] picha ya chain a barafu.