- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Sinagogi Pekee Lililobaki Myanmar

Mada za Habari: Asia Mashariki, Myanmar (Burma), Dini, Historia, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia

Lilijengwa miaka 120 iliyopita, Sinagogi [1] la Musmeah Yeshua lililoko eneo la Yangon ni Sinagogi pekee la wayahudi lililoyobaki katika eneo linaloongozwa na waumini wa dini ya Kibudha waishio nchini Myanmar. Mbali na kuwa kivutio cha utalii, pia limetajwa kama jengo la urithi la mambo ya kale katika mji huo.