- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Pongezi kwa Waziri Mkuu Mpya wa Nepal

Mada za Habari: Asia ya Kusini, Nepali, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala

Bunge la Nepal limemchagua Bw. Sushil Koirala (75) [1], rais wa chama cha Nepali Congress, kuwa Waziri Mkuu wa Nepal. Mwanablogu wa NNepali aishiye ughaibuni Indra [2] anampongeza Waziri Mkuu mpya na anafikiri kwamba “zawadi aliyonayo Bw. Koirala kwa kuwawezesha wengine kwa unyenyekevu na ukweli haitaondoka wa haraka”.