- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

PICHA: Wavenezuela Waishio Ng'ambo Waungana na Waandamanaji

Mada za Habari: Venezuela, Maandamano, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vita na Migogoro

Maelfu ya Wavenezuela wanaoishi ng'ambo wameandaa maandamano kuwaunga mkono wenzao wanaoandamana mitaani [1] katika nchi yao ya Bara la Amerika ya Kusini. Picha ya mikusanyiko hiyo zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye ukurasa wa Facebook uitwao SOS Venezuela [2] [es] picha nyingi zinakusanywa, ambazo pia zinachapishwa kwa alama habari ya #iamyourvoicevenezuela [3] #SOSVenezuela [4] na #PrayForVenezuela [5] kwenye mtandao wa Twita na Instagram.

Mpwa wangu amenitumia picha hii ya Wavenezuela na wageni wanaoandamana leo mjini Malta.

Baadhi ya Wavenezuela ng'ambo walitumia fursa ya maandamano hayo kupeleka nyaraka kwa mashirika ya kimataifa au mabunge ya nchi hizo wanakoishi. Hivi ndivyo walivyofanya raia walioandamana mjini The Hague.

Wavenezuela jijini The Hague, Uholanzi. Tulipeleka nyaraka kwenye Bunge. Tulilaani vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu nchini Venezuela

Gaby Silva [13] aliweka video kwneye mtandao wa Instagram [14] [es] inayoonyesha maandamano yaliyofanywa na kikundi cha Wavenezuela jijini Madrid. Video hiyo inawaonyesha wananchi hao wakitoa mwito wa haki, amani na majadiliano.

Gazeti la TalCual [15] [es] lilisambaza picha ya waandamanaji kwneye viwanja vya Times Square jijini New York.

MAANDAMANO JIJINI NEW YORK. Mamia ya Wavenezuela waliandamana kwenye viwanja vya Times Square.

Kulikuwa na maandamano pia nchini Australia:

Wavenezuela jijini Sydney walionyesha mshikamano wao kuunga mkono maandamano ya wanafunzi

Wakati huo huo, nchini Venezuela kiongozi wa upinzani Leopoldo López [22] alitekeleza ahadi yake kwa kujisalimisha mwenyewe kwa [23] mamlaka za serikali na Rais Nicolás Maduro alitangaza [24] kwamba atakabiliwa na mashitaka ya uchochezi na “kutokuelewa Katiba”.