Huku ukiwa umepangiliwa ufanyike mwanzo wa kipindi cha pili cha Rais Park Geun-hye madarakani, takribani wa-Korea elfu 40 (polisi wanadai ni elfu 15) walifanya mgomo [1] nchini kote. Mgomo huo, ulipangwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Korea [2], ukiwa na wito wa kusitishwa kwa kudhibitiwa kwa vyama vya wafanyakazi, hatua ya serikali kubinafsisha sekta ya umma na kufunikwa skandali ya wizi wa kura katika uchaguzi wa rais [3]. Mwandishi wa habari za kiraia anayeheshimika Mongu alitwiti picha [4] ya maandamano (imewekwa hapa chini). Picha zaidi zinaweza kupatikana kwenye ukurasa wa Facebook wa chama cha wafanyakazi [5] [ko].
국민파업. 서울광장 안입니다. 꽉 찼습니다. pic.twitter.com/ZwdJ9AFlYh [6]
— 미디어몽구 (@mediamongu) February 25, 2014 [4]
Mgomo mkubwa, kwenye Ukumbi wa Seoul City Hall Plaza. Ulijaa vilivyo.