Vadim Makhorov na Vitaly Raskalov walisisimua watu kupitia mtandao wa intaneti mnamo tarehe 12 Februari, 2014 pale walipotuma video wakiwa wanapanda Mnara wa Shanghai. Mnara wa shanghai wenye urefu wa futi 2,073 (mita 632), utakapokamilika utakuwa ni mnara wa pili kwa urefu duniani baada ya Burj Khalifa ulioko Dubai.
Hiyo ndiyo Shanghai ilihojiana na jopo la Warusi hao kuhusiana na kupanda kwao mnara huu.
Zifuatilie picha hizi za kuvutia ambazo wawili hawa walizipiga wakiwa katika kilele cha mnara wa Shanghai pamoja na picha nyingine za jiji la Shanghai. Picha zote kwa idhini ya Vadim Makhorov na Vitaly Raskalov wa On the Roofs. Picha zilichapishwa tena kwa ruhusa.