- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Picha Mpya ya Korea Kaskazini ya Shirika la Anga la Marekani

Mada za Habari: Asia Mashariki, Korea Kaskazini, Korea Kusini, Mahusiano ya Kimataifa, Sayansi, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Upiga Picha

Wasomaji wa kimataifa wanaofuatilia masuala ya Korea Kaskazini labda wangekutana angalau mara moja na picha hii maarufu ya rasi ya Korea [1] kutoka Shirika la Anga la Marekani (NASA) kuonesha tofauti kubwa ya taa zinazoangaza usiku kwenye nchi hizo mbili za Korea. NASA hatimaye walihuisha picha zao za Satelaiti [2] na ‘ina mwonekano mzuri kuliko picha ya zamani ya NASA’, inaandika blogu ya Teknolojia ya Korea Kusini [3]. Blogu hiyo pia inatambulisha toleo la video la picha hiyo [4] linaloonyesha  Korea Kaskazini katika mukhtadha wa eneo lote la Asia Kaskazini.