Nionyesheni ‘Katiba Inayotokana na Mnyama’, Adai Rais wa Zambia

Wakati maswali yakianza kuibuka kuhoji utashi wa kisiasa wa Rais wa Zambia Michael Sata kufuatia ahadi ya kampeni kusimamia mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya, kiongozi huyo amekuja na mzaha akikejeli “kelele” za wanaotaka katiba “inayotokana na watu” na kuwauliza kama ipo nchi yoyote duniani imewahi kupitisha katiba iliyotokana na wanyama.

Wakati wa sherehe za kuapishwa kwa maafisa wa masuala ya katiba, wakati pekee ambapo Sata amewahi kulihutubia taifa kwa njia ya runinga, alisema:

Na kwenu nyote mlioko hapa, hebu mwulizeni mwanawake aliyesoma kuliko wote hapa, [kaimu Jaji Mkuu] Mheshimiwa [Lombe] Chibesakunda. Siku zote nawasikia mnasema katiba inayotokana na watu, katiba inayotokana na watu. Mheshimiwa, wapi tutapata katiba inayotokana na wanyama? […] Umewahi kuiona katiba inayotokana na wanyama, nchi gani kwa sababu kila mtu [naona] anazungumzia katiba iliyotokana na watu, ili ukishatengeneza ile iliyotokana na mnyama, labda tumwulize Bw. Phiri, tukishatengeneza katiba iliyotokana na wanyama, tuweze kuzilinganisha katiba hizo mbili, kile kilichomo ili sasa tuweze kutazama cha kufanya..

Kama chama cha upinzani, sasa kikiwa chama tawala nchini Zambia, chama cha Patriotic Front kilikishinda kilichokuwa chama tawala cha Movement for Multiparty Democracy (MMD) mwaka 2011 kwa ahadi kuwa kikichaguliwa kuingia ikulu baadae mwaka huo, kingepitisha katiba mpya ndani ya siku 90 baada ya kutwaa madaraka.

Wiki kadhaa baada ya kushika madaraka, Rais Sata aliteua kamati ya ufundi ili kutazama michakato iliyotumika kutengeneza katiba zilizopita ili kuja na rasimu ya katiba mpya. Pendekezo hilo ambalo ni la pekee lilikuwa kwamba rasimu hiyo ya katiba ingetolewa kwa wakati mmoja kwenda serikalini na kwa wananchi na wakati huo huo kura ya maoni ingefanyika.

People holding a banner demanding that President Sata releases the draft constitution. Picture used with permission of The Zambian Voice.

Watu wakiwa wamebeba bango wakidai kwamba Rais sata aitoe rasimu ya katiba. Picha imetumiwa kwa ruhusa ya The Zambian Voice.

Huku kukiwa na tarehe za mwisho zinazobadilika badilika na hatimaye mchakato wa kutengeneza katiba ukiendelea kwa mwaka wa pili sasa, serikali ilibadilisha mbinu yake na kuiomba kamati ya ufundi kuchapisha nakala kumi pekee za rasimu ya katiba, ili baraza la mawaziri lipate fursa ya kuiptia kwanza. Rasimu hiyo ya katiba baadae ilivuja kupitia blogu ya Zambian Watchdog na sasa inafahamika kama “nakala ya kumi na moja”.

Baadhi ya watu walianza kuwa na wasiwasi na utashi wa kisiasa wa Rais Sata katika kuleta katiba mpya pale alinukuliwa akisema, nchi hii haikuhitaji katiba mpya kabisa bali mabadiliko ya hapa na pale. Wakati mwingine, Sata alisema katiba ya sasa ilikuwa bado ni nzuri kwa sababu chaguzi sita zilishafanyika kwa kuitumia katiba hiyo hiyo.

Nyalubinge Ngwende katika blogu yake inayojulikana kama Brutal Journal  aliandika:

Linapokuja suala la katiba, Rais sata asitufanye wajinga. Ujenzi wa barabara, vyuo vikuu, shule zaidi na huduma za afya hazitakuwa na maana yoyote kama raia wanakuwa mateka wa utawala wa kisiasa unaokataa kuwapatia yenye maana ya kuwapatia uhuru wao kamili na fursa pana kwa raia, bila kujali waliko kijiografia katika ramani ya dunia. 

 Katiba inayotokana na watu ni chaguo letu na sio chaguo la PF! 

Ngwende anaendelea kuelea kile kinachomaanishwa na katiba inayotokana na watu katika nchi ambayo Baraza la Mawaziri linaloongozwa na rais limefanya wajibu wake vya kutosha katika kutengeneza katiba kwa njia ya kutoa vipengele ambavyo wananchi walivipendekeza na kuviondoa vile vinavyowapendelea watawala:

Wakati wanaharakati wa asasi za kiraia wanazungumzia katiba iliyotokana na watu, wanamaanisha katiba nzuri itakayodumu kwa muda mrefu; yenye sheria zinazojibu matakwa ya watu na ile ambayo watu wenyewe wataikubali.

Akiungana na wanasiasa wengine wa upinzani na asasi za kiraia, rais wa MMD Nevers Mumba alikuwa na maoni haya:

Ninafikiri kuwa Mungu amemruhusu [Rais Sata] apoteze mwelekeo kwa sababu siwezi kuamini Rais akitoa matamshi ya aina ile. Kile ambacho Wazambia wanakisema ni kwamba tazama, tunahitaji katiba bora ambayo tutashiriki katika kuitengeneza […] Kitendo chake [Rais Sata] kutoa matamshi ya aina ile yanaonyesha kiburi cha hali ya juu sana. Ninamwomba rais kuwa na hadhi ya ki-Rais katika suala hili. [Wananchi] tumekusudia kupata katiba mpya, iwe akiwepo yeye au vinginevyo.

Sata aliwaamuru maafisa wa serikali kutokujibu lolote linalohusiana na mjadala wa katiba. Hata hivyo, Waziri wake wa Sheria na Katibu Mkuu wa PF Wynter Kabimba akiwa kwenye ziara nchini Malawi huenda alipuuzia woga wa serikali wa serikali yake kwenye rasimu ya katiba -[hasa kipengele kinachotaka] kufikiwa kwa asilimia 50 ya kura zote jumlisha kura moja kwa uchaguzi wa rais na mgombea mwenza wake wa nafasi ya umakamu wa Rais. Kabimba alisema:

Kuna madai yote haya kuhusu hitaji la kikatiba la asilimia 50 jumlisha kura moja na hitaji la mgombea mwenza bila kuzingatia kuwa mambo haya yanapokuwa kwenye katiba yamesababisha matatizo mengine zaidi kuliko majibu ambayo [vipengele hivyo] vingetoa kwa jamii.

Tunaweza kujifunza kwa wengine. Hatulazimiki kufanya makosa yale yale ambayo wengine wameyafanya nia [yetu ikiwa ni] kufanya jambo jema zaidi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.