Mwandishi wa Habari Mwingine afariki Nchini Mexico: Gregorio Jiménez de la Cruz

Maafisa wa serikali nchini Mexico wamethibitisha kuuawa kwa Gregorio Jiménez de la Cruz, ajulikanaye pia kwa jina la “Goyo”.

Mwili wa Jiménez de la Cruz ulikutwa katika makaburi la siri tarehe 11, Februari, 2014, hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka El Universal [es] na La Jornada. [es] [Habari hii kwa Kiingereza iliyoandaliwa na BBC inapatikana hapa]

Gazeti la kielekroniki la kila wiki la Proceso [es] mapema lilitoa taarifa ya kupotea kwa mwandishi huyu wa habari huku likihitaji majibu kutoka serikalini.

Katika ukurasa wa Twita, kiungo habari #HastaQueAparezcaGoyo [es] kilitumika kama namna ya kuiunga mkono familia na marafiki wa Jiménez de la Cruz wakati wa kipindi kigumu walichopitia.

Mwandishi wa habari, Paola Rojas ndiye aliyekuwa wa kwanza kusambaza habari katika kupitia ukurasa wa Twita:

Mpelelezi maalum wa shitaka la Veracruz amethibitisha kuwa mwandishi wa habari Gregorio Jiménez aliuawa

Mwanaharakati, Jesús Robles Maloof alimtaka Gavana wa jimbo la Veracruz kujiuzulu, mahali ambapo Gregorio Jiménez de la Cruz alifanyia shughuli zake kama mwandishi wa habari:

Ni muda muafaka wa Javier Duarte aondolewe katika serikali.

Asubuhi ya Februari 11, mwanaharakati mmoja aliweka picha hii katika ukurasa wa Twita:

Pia, mtumiaji wa Twita, Másdel131 aliweka picha iliyopigwa kutoka kwenye maandamano hayo:

Kutoka makao makuu ya serikali ya Veracruz, waandishi wa habari waandamana

Pertaesus aliuliza:

Hitaji lao lililowekwa katika kiungo habari #HastaQueAparezcaGoyo laibua swali jingine lenye kuibua maumivu- itachukua muda gani hadi kuirudisha nchi yetu?

Kwa mujibu wa Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka, “Mexico ni moja ya nchi hatari sana duniani kwa maisha ya waandishi wa habari”, Umoja huu unaongeza kuwa, “Zaidi ya waandishi wa habari 80 wameshauawa katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, 17 hawajulikani walipo”  Kifo cha Gregorio Jiménez de la Cruz  lazima kijumuishwe katika idadi hii.

Nchini Mexico, kuna hali ya vita iliyoshindikana na machafuko, hii ni tokea Rais aliyepita, Felipe Calderón, kuanzisha mkakati wa kukabiliana na madawa ya kulevya mnamo mwaka 2006. kwa kuzingatia kifo cha Gregorio Jiménez de la Cruz, machafuko nchini Mexico yanaendelea chini ya uangalizi wa Enrique Peña Nieto.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.