- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mrembo wa Venezuela Auawa kwa Risasi Wakati Akiandamana

Mada za Habari: Amerika Kusini, Venezuela, Habari za Hivi Punde, Maandamano, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia

Génesis Carmona, mwanamitindo wa Venezuela, mwathirika mwingine wa vurugu za kisiasa.

Génesis Carmona, mrembo wa Venezuela na mwanafunzi, ameuawa [4] [es] mnamo Februari 19 kwa jereha lililotokana na risasi ya kichwani iliyompata [5] [es] jana wakati wa maandamano [6] ya kuipinga serikali.

Hivi ndivyo walivyomsafirisha Génesis Carmona aliyepigwa risasi ya kichwa wakati akiandamana jijini Valencia.

@pabloaure akiwa kwenye kliniki ya Guerra Mendez akizungumza na mama na mwanafamilia mwingine wa Genesis Carmona mwenye jeraha la risasi kichwani.

Kwa mujibu wa madaktari bingwa waliomtibu kwneye kiliniki hiyo ya Dk. Rafael Guerra Méndez iliyopo jijini Valencia, Mrembo huyo ambaye ni Miss Tourism wa Carabobo kwa mwaka 2013 alipigwa risasi kutoka upande wake wa kulia wa fuvu, linalobeba sehemu ya ubongo inayohusika na kuona. Kulikuwa na tetesi kuwa angepoteza uwezo wake wa kuona hata kama angeweza kupona.

Genesis Carmona (23) amejeruhiwa na risasi akiwa kwenye maandamano jijini Valencia ametoka kwenye chumba cha upasuaji, na sasa yu katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Gazeti la Caracas lilichapisha mkusanyiko wa twiti [14] [es] kutoka kwa mtumiaji wa mtandao wa twita aitwaye Héctor Rotunda (@Hecalo [15]), anayeelezea mfululizo wa matukio tangu Génesis Carmona alipopigwa risasi mpaka alipopoteza maisha yake. Rotunda alikuwa karibu na mrembo huyo wakati wa maandamano hayo.

Tulikuwa tukiandamana mbele ya kituo cha basi cha Cedeño. Tulisikia mlio wa risasi na wote tukalala chini…

Kwenye mtandao wa twita miitikio [17] ya tukio hilo pamoja na lawama zinaendelea kumiminika. Gavana wa Jimbo la Carabobo, Francisco Ameliach, ametwajwa kuwa mtu aliye nyuma ya shambulizi hilo kwenye maandamano jijini Valencia. Siku chache zilizopita Gavana huyo alituma twiti kwenye mtandao wa twita kwamba waandamanaji sasa wamezoea kumtuhumu kwa kuanzisha mapigano [18] [es]. Katika twiti ifuatayo, kwa mfano, anataja UBCH [19][es], kifupi cha Kikosi cha Vita cha Bolívar – Chávez (Unidades de Batalla Bolívar – Chávez) cha Chama cha Kisoshalisti cha Venezuela (PSUV [20] – Partido Socialista Unido de Venezuela), ambacho ndicho kinachotawala nchini humo.

UBCH muwe tayari kwa kujibu mapigano. Diosdado atatoa amri.

Diosdado Cabello [24] ndiye Rais wa Bunge la Taifa hilo Venezuela.

Wakati huo huo, mbunge Francisco Soteldo alitoa kauli [25] [es] kwenye vyombo vya habari akidai haki itendeke kufuatia kifo cha Carmona:

Soteldo: “Tunadai haki kwa kifo cha Génesis Carmona”

Kwa kifo hicho, Carmona anakuwa mtu wa nne kupoteza maisha katika maandamano [6] ambayo yamekuwa yakiendelea nchini Venezuela.