- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Misri: Kupandishwa cheo kwa Sissi ni ya Hutua ya Kuelekea URais?

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Misri, Habari za Hivi Punde, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi

Rais wa serikali ya mpito ya Misri, Adly Mansour atoa amri ya Rais ya kumpandisha cheo Jenerali Abdel Fattah El-Sissi, ambaye ni waziri wa ulinzi kuwa Jemadari Mkuu. Hii ni nafasi ya juu kabisa katika jeshi la Misri

Upandishwaji cheo huu umezua mjadala mkubwa katika mitandao ya intaneti ambapo watu wengi wanajiuliza kama ndio njia ya Sissi kugombea urais unaotarijiwa kufanyika mwisho wa mwezi Aprili.

Adam Makary katika ukurasa wa Twita aandika:

Louisa Loveluck atoa angalizo:

Pia, Ahmed Abrass anafafanua maana ya cheo cha Jemadari Mkuu [ar]:

” Kwa kiingereza, Jemadari Mkuu ina maana kuwa mtu Fulani aliyewangoza wanajeshi vitani na akapata ushindi mkubwa .”

Kwa El Siss, hili si jambo la yeye kulitilia maanani. Hata hivyo, inaonekana kuwa kuwa Jemadari Mkuu siyo kigezo cha muhimu katika jeshi la Misri na hata hivyo Meja Jenerali huyu mstaafu alikuwa na vigezo vyote vya kumfanya kuwa Jemadari Mkuu .

Nervana Mahmoud afafanua:

Bel Trew athibitisha kuwa:

Na Egyptian Streets asema:

Watumiaji wengi wa mtandao wameonesha kushangazwa na waziwazi kuchukizwa na habari hii.

Katika mtandao wa kijamii wa Facebook, Mina Labib auliza [ar]:

يتكافؤه على ايه ؟؟ علي إنفجارات ؟؟!!

Anatunukiwa hasa kwa lipi alilolifanya? Kuhusu milipuko iliyotokea?

Januari 24, Misri ilikabiliwa na mfululizo [10] wa milipuko iliyoua watu sita na wengine 70 walijeruhiwa huko Cairo.

Baadhi ya watu wanaona kuwa, kupandishwa cheo huku ni namna ya ya haraka ya Sissi kuelekea kugombea Urais. Nervana Mahmoud aandika:

Egyptian Streets adds:

Na pia, mwanahabari Patrick Kingsley anafafanua:

Inaonekana kuwa kugombea Urais siyo sababu pekee ya kupandishwa cheo hiki. Tarik Salama atwiti:

Basil Al Dabh anaongeza:

Katika kipindi cha taharuki na kutokujali uhuru wa mtu, baadhi ya watu wanaokuwa hii ni hatua nyingine kuelekea kuheshimu watu kama Mungu wao na kuwapenda, mfumo ambao viongozi wa Misri wamekuwa wakiusimamia.

Zack Gold afafanua:

Gr33ndata akiweka kikaragosi: