- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Fuatilia Kuenea kwa Maandamano ya Ukraine

Mada za Habari: Ukraine, Habari za Hivi Punde, Haki za Binadamu, Harakati za Mtandaoni, Maandamano, Mahusiano ya Kimataifa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala

Posti hii ni sehemu ya Habari zetu maalumu kuhusu  Maandamano ya Ukraine [1].

Maandamano ya Ukraine yamekua kiasi cha kufikia hatua ya mapambano kati ya mamia ya maelfu ya raia na vikosi vya serikali jioni ya Februari 18. Barabara zinazoelekea jijini zilikuwa zimefungwa na mamlaka za serikali, na treni za jiji la Kyiv zilisimamisha huduma zake. Kituo kikuu cha televisheni kinachopingana na serikali kinaripotiwa kufungiwa kurusha matangazo yake. Mapigano makali kati ya polisi na waandamanaji katika viwanja vikuu vya mikusanyiko ya watu jijini humo yaliendelea mpaka usiku. Mnamo tarehe 19 Februari, maandamano ya Kyiv  yaliripotiwa [2] kupoteza maisha ya watu wasiopungua 25 na wengine zaidi ya 1,000 wakijeruhiwa.

Asubuhi ya Februari 18, 2014, wapinzani wa serikali walijaribu kuwasilisha muswada Bungeni ili kurudisha toleo la zamani la Katiba ya nchi hiyo, ambalo lilidhibiti mamlaka ya rais. Hatua hiyo iliungwa mkono na harakati za Euromaidan ambazo kwa sasa zimetimiza miezi mitatu, ambazo zinaendesha maandamanokila siku kwenye majiji kadhaa kote nchini Ukraine kudai serikali ya Rais Viktor Yanukovych kuondoka madarakani. 

Hapo awali, waandamanaji waliandamana kuelekea kwenye jengo la Bunge. Wakati spika wa bunge alipokataa kupokea muswada huo, mapigano yalianza kati ya raia na polisi. Wabunge wanaomwunga mkono Rais Yanukovych tayari walikuwa wameshaondoka kwenye jengo la Bunge, wkaati rais mwenyewe aliingia mitini. Polisi na vikosi vya ulinzi vilivamia viwanja vya Maidan Nezalezhnosti ambavyo ni ngome ya waandamanaji.

A screencap from Maidan Nezalezhnosti [Independance Square] in central Kyiv, Ukraine. Feb. 19, 2014

A screenshot from Maidan Nezalezhnosti [Independance Square] in central Kyiv, Ukraine. Feb. 19, 2014

Rais Yanukovych ametoa kauli  akiwalaumu wapinzani [3] kwa vurugu na ghasia zilizoilazimu polisi kuingilia kati. Mazungumzo yaliyodumu kwa usiku mzima kati ya waandamanaji na serikali yalikwama na waandamanaji kwa mara nyingine waliruhusiwa kutumia viwanja vya Independence Square jijini Kyiv mnamo Februari 19.

Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso alitoa  tamko kwa njia ya video [4] kuhusiana na hali ya mambo ilivyo nchini Ukraine na pia alitwiti:

Nafuatilia kinachoendelea nchini #Ukraine [5] kwa tahayaruki na mshangao. Tunatarajia hatua zilizokubaliwa na #Umoja wa Ulaya [6] zitachukuliwa haraka sana.

Vyombo vya habari vya kiraia na vile vilivyohuru bado vinatumia zana za mtandaoni kuhabarish kile kinachoendelea nchini humo na kwa ajili ya kupata habari za yanayojiri kwa ajili ya kuzitangaza kwa ulimwengu. Habari za moja kwa moja kuhusu maandamano na mapigano kutoka Kyiv zinapatikana katika vyanzo kadhaa vya mtandaoani:

RFE/RL: http://www.youtube.com/watch?v=ObBHW8XQvUQ [9]
Espreso-TV: http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=Y_LFrMcoEm4 [10]
SpilnoTV: http://www.ustream.tv/channel/16555296 [11]
HromadskeTV: http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=dh3_1L9XO60 [12]
UkrStreamTV: http://www.ustream.tv/channel/16573315 [13], http://www.ustream.tv/channel/17251372 [14]

Twita ni uwanja maarufu pia kwa kufuatilia habari mpya zinazokuja kutoka Kyiv. Global Voices imeorodhesha akaunti za mtandao wa twita zinazotumia lugha ya kiingereza kuandika yanayoendelea nchini Ukraine:

https://twitter.com/zeitonline/lists/ukraine [15]
https://twitter.com/ckaratnytsky/lists/ukraine [16]
https://twitter.com/juliacreinhart/lists/ukraine-russia [17]
https://twitter.com/zeynep/lists/ukraine [18]
https://twitter.com/rm867/lists/ukraine-euromaidan [19]

Watafsiri wa kujitolea wa Euromaidan wamekabiliwa na shughuli nyingi kuliko ilivyowahi kuwa, wakitafsiri habari mpya nyingi kadri iwezekanavyo kutoka kwenye maeneo yanakofanyikia maandamano. Blogu maarufu zaidi na ukurasa wa Facebook ni ule wa Tafsiri za Maidan:

http://maidantranslations.wordpress.com/ [20]
https://www.facebook.com/EuroMaydanTranslations [21]

Habari mpya kutoka kwa waandaaji wa maandamano, waliopewa jina la utani la “Makao Makuu ya Euromaian”, wanaweza kufuatiliwa katika ukurasa wao wa Facebook katika Lugha ya Kiingereza:

https://www.facebook.com/euromaidanpr [22]