Habari kutoka 23 Februari 2014
Wamalagasi Wajadili Kivazi na Maoni ya Mlimbwende wa Kigeni Kuhusu Madagaska
Picha ya Tangazo la Kivazi cha Kuogolea 2014 iliyopigwa eneo la (kisiwa cha) Nosy Iranja, Madagaska: Nosy Iranja ni kisiwa kinachofahamika kama Turtle kwa sababu viumbe waitwao Hawksbill Turtles walikuja ufukweni kutaga mayai yao. Kisiwa hicho pia kinafahamika kwa mchanga wa pekee unaounganisha visiwa hivyo viwili. Mlimbende mashuhuri wa ki-Rusi...
Tafakuri kwenye Mkutano Mkubwa Zaidi wa Blogu Nchini India
#WIN14, mkutano mkubwa zaidi na tuzo zinazoongoza nchini India, unaoandaliwa na BlogAdda, ulifanyika Februari 89, 2014. Mwanablogu Dk. Roshan Radhakrishnan, aliyeshinda tuzo ya blogu bora ya uandishi wa ubunifu nchini India, anatoa maoni na picha zake.
Pongezi kwa Waziri Mkuu Mpya wa Nepal
Bunge la Nepal limemchagua Bw. Sushil Koirala (75), rais wa chama cha Nepali Congress, kuwa Waziri Mkuu wa Nepal. Mwanablogu wa NNepali aishiye ughaibuni Indra anampongeza Waziri Mkuu mpya na anafikiri kwamba “zawadi aliyonayo Bw. Koirala kwa kuwawezesha wengine kwa unyenyekevu na ukweli haitaondoka wa haraka”.
Mwandishi Mwandamizi wa Kichina Akosolewa kwa Kujifungulia Marekani
"...anachotaka tu ni mwanae awe na mtindo wa kawaida wa maisha, kitu ambacho hakina uhusiano na uzalendo. Labda, hili ndilo tatizo ambalo serikali yapaswa kulitafakari..."
Waandishi wa Habari za Kiraia, Jiandikishe Kupata Video Bure
Jukwaa linalokusanya video kadri zinavyowekwa mtandaoni linaloitwa Ustream linalota fursa ya kujiandikisha kufungua anuania mpya na pia kuzitangaza kwa ajili ya kuzitumia video hizo kwa ajili ya habari zinazotokea, uanaharakati na hata kwa matumizi ya mengine ya faida kwa jamii. Hivi karibuni Ustream imesaidia chaneli tatu za moja kwa moja...