- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Uvumbuzi: Kompyuta Inayotumia Nishati ya Jua Nchini Mali

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Mali, Elimu, Habari Njema, Harakati za Mtandaoni, Maendeleo, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchumi na Biashara
Limmorgal, a low power PC made in Mali via Tech of Africa with permission  [1]

Limmorgal, Kompyuta inayoendeshwa kwa nishati ya jua iliyotengezwa nchini Mali na Kampuni ya Tech of Africa kwa ruhusa

Kama sehemu ya mfululizo wetu juu ya teknolojia na ugunduzi unaofanyika Afrika, hivi karibuni tulionyesha Mashine ya Kuchapishia picha zenye umbo halisi yaani 3D iliyotengenezwa kutokana na taka pepe nchini Togo [2] na mashine ya kukagua usahihi wa maneno katika lugha ya spell ki-Bambara [3]. Leo, tunawaletea kompyuta ya kwanza kutumia umeme mdogo iliyotengenezwa nchini Mali. Kompyuta hiyo inayoitwa Limmorgal (ikiwa na maana ya kikokotozi kwa lugha ya ki-Peul) ni zao la bongo za vikundi viwili vya raia wa Mali, Jumuiya ya Intaneti Mali (ISOC Mali) na Intelec 3. Mamadou Iam Diallo, rais wa ISOC Mali, anaeleza mahitaji wanayohitaji kuyatatua kwa kutumia kompyuta hiyo [4] akiongea na Blogu ya Bamako[fr]:

Nous avons conçu cette machine pour contribuer à la réduction du fossé numérique, mais également à la vulgarisation de l’outil informatique surtout en milieu scolaire. Limmorgal est aussi un ordinateur adapté à l’alimentation par l’énergie solaire grâce à sa faible consommation d’énergie.

Tulibuni kompyuta hii kusaidia kupunguza pengo kati ya walio mtandaoni na wale wasiomudu huduma za kidijitali, lakini pia  upanuzi wa matumizi ya kompyuta mashuleni. Limmorgal ni kompyuta ilitengenezwa mahususi kutumia umeme wa nishati ya jua na inatumia nishati kidogo sana (Watt 24 tu zinahitajika).

Sifa za kompyuta hiyo ni kama ifuatavyo :