- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Shindano la Kuchochea Uanzishwaji wa Biashara Mpaya Nchini Madagaska

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Madagaska, Habari Njema, Mawazo, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchumi na Biashara

Harinjaka, mwanzilishi wa mradi wa Habaka na mwanablogu anayeishi Madagaska, ameanzisha Shindano la biashara mpya Antananarivo 2014 [1] [fr] lenye lengo la kuchagua na kuunga mkono wazo la biashara nchini Madagaska. Anaamini kwmaba kuna  mustakabali mzuri kwa ujasiriamali na ubunifu [2] [fr] nchini Madagaskari. Hapa unaweza kuona tangazo la tukio hilo[fr] :   

"The objective of the Start Up Cup is to connect founders with business investors and VCs." on the Facebook Page of the event  [3]

“Lengo la Shindano hilo la miradi mipya ni kuwaunganisha waanzilishi wa biashara hizo na wawekezaji na wadau wengine” kupitia Ukurasa wa Facebook wa tukio hilo kwa ruhusa