- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Rais wa Korea Kusini Aapa Kupambana Uzushi Unaoenezwa katika Mitandao ya Kijamii

Mada za Habari: Asia Mashariki, Korea Kusini, Habari za Hivi Punde, Harakati za Mtandaoni, Maandamano, Siasa, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Utawala

Je, serikali ya Korea Kusini imejiandaa kwa kufuatilia mitandao ya kijamii? Matamshi ya hivi karibuni ya Rais Park (full transcript [1] [ko]) yamewashitua wa-Korea wanaotumia mtandao. Park, akiwalenga “uvumi ule unaosambaa kupitia mitandao ya kijamii”, alisema “kama serikali ikiachia mambo haya yakaendelea, itakuwa ghasia nchi nzima” na kuongeza “kumbukeni mamlaka za nchi zinahitaji kuchukua hatua kwa haraka sana na  kwa hisia zinazotakikana dhidi makundi yale yanayoharibu hali ya hewa”. Watumiaji wengi wa mtandao wa twita walipigia kelele wasiwasi wao na kuonyesha ukweli (kama twiti ya @ppsskr [2] [ko] ambayo ilizunguka zaidi ya mara 500) kwamba vyombo vya serikali vimelituma zaidi ya twiti milioni 24 ili kumpa nafuu Park [3]  wakati wa uchaguzi wa rais uliofanyika hivi karibuni.